KAMPUNI ya simu za mikononi ya Zain Tanzania leo imechezesha bahati nasibu yake ya ‘Jivunie SMS’ na kupata washindi wawili watakaopewa tiketi za kwenda kuangalia fainali za Kombe la Dunia zinatakazoanza Juni 11 mwaka huu nchini Afrika Kusini.
Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam, Meneja Uhusiano wa Zain, Mutta Muganyizi, alisema kwamba kila mshindi atapata fursa ya kusafiri na mtu yeyote mmoja atakayependa kwenda naye huko Afrika Kusini.
Washindi hao ni Joseph J. Semali (32) mkazi wa jijini Dar es Salaam, Bokeloo Athuman (49) mkazi wa Kabuku, Tanga. Wengine waliojishindia 500,000/= kila mmoja ni Osele D. Gilina (20) mkazi wa Temeke jijini Dar es Salaam na Justine Benda (38) mkazi wa Pugulu, Mtwara.
Mutta pia aliwaomba wateja wote waendelee kutuma meseji kwa wingi ili waweze kupata nafasi za kushinda zaidi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment