Social Icons

Tuesday, June 1, 2010

JACK PEMBA ALIKUWA MGENI RASMI JAM SESSION


Find more photos like this on G5 world
PEDESHE wa ukweli kunako pande za burudani mwenye makazi yake nchini Uingereza Jack Pemba hivi juzikati aliibuka Club Sun Cirro iliyopo eneo la Lego Sinza jijini Dar es Salaam katika mchakato mzima wa Jam Session akiwa ndiye mgeni rasmi siku hiyo.

Akiwa katika shughuli hiyo Jack Pemba alipata fursa ya kusaini baadhi ya Tiketi za washiriki wa ishu hiyo na baadaye kupiga nao stori mbili tatu za kuwapa moyo washiriki huku akiwaomba waongeze bidii katika masomo yao ili baadaye waweze kuwa na maisha bora na mazuri kama yake.

Baada ya kumaliza kuwapa mawaiza hayo aliwakabidhi waandaaji wa Jam Session iliyo chini ya Hartman Mbilinyi kitita cha Tsh, Milioni moja ikiwa ni moja ya mchango wake baada ya kuvutiwa na maandalizi ya mpango huo pia alitowa Laki mbili kwa Mr & Miss Jam Session kwaajili ya kuwawezesha kufanya shopping za mavazi yao.

Uzinduzi rasmi wa Jam Session utakuwa June 6 Mwaka huu ndani ya Club Sun Cirro Sinza jijini Dar es Salaam ambapo wasanii kibao wa watatumbuiza akiwemo Michael Rose kutoka nchini Uganda,Mhesimiwa Temba TMK, Chege Chigunda ‘Mtoto wa mama Said na wengine kibao.

1 comments:

Mateja said...

yap iko poa sanaaaaaaaa