Social Icons

Friday, May 21, 2010

MASELE CHAPOMBE: DEMU WANGU ANA ‘INYE’ ILA SIYO LA KICHINA!


Mambo vipi wakubwa kwa wadogo? Ni matumaini yangu kuwa mko poa sana na hapa tunaendeleza libeneke lile lile, yaani burudani.
Baada ya wiki iliyopita kuwa na mmoja wa mapresenta wa program ya Leo Tena kunako Redio ya Watu, Cloud FM, Zamaradi Mketema, wiki hii tunamleta kwenu ‘Komediani’ wa Kundi la Mizengwe linalovunja mawingu kupitia Kituo cha Runinga cha ITV, Crispine Masele ‘Masele Chapombe’.

Masele ni mzaliwa wa Shinyanga, lakini alikulia pande za Iringa na Dar kufuatia hamahama ya wazazi iliyokuwa ikisababishwa na kazi. Kwa sasa Masele anaishi pande za Mikocheni A, jijini Dar akipiga mzigo wa kurekodi filamu za vichekesho. Mbali na kazi hiyo, pia jamaa ni mfanyabiashara wa mitumba katika sehemu mbalimbali za Jiji la Dar. Ili kupata kitu kamili ungana naye akijibu sindano kumi za moto za safu hii.

TQ: Unaweza kukumbuka ni lini ulianza kufanya kazi za usanii na ni nini kilichokuvutia hadi ukajiingiza huko?

MASELE: Kazi ya sanaa niliianza mwaka 2005 nilipoamua kujiunga katika Kikundi cha Dar Talent kilichokuwa na maskani yake jijini Dar es Salaam. Sanaa hiyo nilikuwa nayo moyoni toka siku nyingi kwani nilikuwa nikijiona mwenye kipaji hicho tangu kitambo.

TQ: Kwanini uliamua kutumia stahili ya kuwa mlevi hadi ukapachikwa jina la Masele Chapombe?

MASELE: Nilipokuwa Dar Talent, mwalimu wangu alinitaka kuonesha kipaji changu cha uchekeshaji. Nakumbuka iliniwia vigumu kwani wasanii wenzangu walikuwa wako juu zaidi kuliko mimi, hivyo siku hiyo nilikosa kitu cha kuigiza kwani sikupenda wote tufanane kwa kuigiza vitu vinavyofanana.

TQ: Kwa hiyo ilikuwaje hadi ukaamua kutumia staili hiyo?

MASELE: Siku hiyo niliporudi nyumbani nilikutana na a jirani yangu ambaye alikuwa amelewa akiwa anazungumza maneno mengi na kufanya mambo mengi ya kuchekesha, lakini pombe ilipokatika, alipoulizwa alishindwa kukumbuka vituko vyote alivyokuwa akivifanya.

TQ: Masele kuna tetesi kwamba una tabia ya kulewa kiukweli. Je, ni kweli?

MASELE: Licha ya kutokuwa mlevi kama wengi wanavyodhani, nimetumia kipaji changu kuigiza hadi sura ya mtu mlevi inavyotakiwa kuwa pamoja na mwili wake na vituko vya walevi, jambo ambalo huwa linawashinda wasanii wengi nchini kwa kuwa wanakosa uhalisia.

TQ: Nini mafanikio yako katika kazi ya sanaa?

MASELE: Mbali na kutambulika, lakini biashara zangu zimekuwa zinakwenda mwake mwake. Sanaa inaniweka mjini chini ya Meneja wangu, John Dickson. Filamu zangu kama Inye Plus, Inye Mbwetembwete na nyingine kibao, zinanifanya niwake mjini.

TQ: Mbali na mafanikio hayo lakini baadhi ya wasanii wakipata chochote kitu hukimbilia kununua vitu vya starehe kama magari na matanuzi mengine. Je, kwako wewe hili likoje?

MASELE: Ni kweli ‘but’ kwa upande wangu niko kwenye maandalizi naangusha bonge la mjengo pande za Mbezi Shamba, jijini Dar.

TQ: Katika kila kazi kuna vigingi na Vikwazo. Je, kwa upande wako hali ikoje?

MASELE: Binadamu na mashabiki wangu wajue kuwa ulevi siyo sababu ya kudharauliwa mtaani au katika jamii. Mara nyingi naambiwa nimelewa wakati mimi niko safi, unakuta hata sijalewa.

TQ: (Swali la kifuta jasho) Masele umeoa?

MASELE: Sijaoa, lakini nina mke mwenye makalio makubwa ‘Inye’ ambaye ni raia wa Italia, mtu na shughuli zake.

TQ: Umesema ana makalio babkubwa, Je, ni ya Kichina?

MASELE: Kile ni kitu orijino, siyo cha Kichina.

TQ: Ni nini matarajio yako ya baadaye na unawaambia nini mashabiki wako?

MASELE: “Natarajia kufanya makubwa katika fani ya vichekesho na filamu kwa ujumla. Mashabiki wangu walikuwa wakinidai filamu yangu, nimefanikiwa kuwapatia filamu hiyo nikiwa nikiwa na wasanii chipukizi sasa nitarudi kuendelea na Mizengwe kama kawaida," anasema Masele Chapombe.

0 comments: