Friday, May 21, 2010
ALLY CHOKI KUTAMBULISHA RASMI EXTRA BONGO MEI 28
Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo ‘Mjini Mipango’ Ally Choki ‘Mzee wa Farasi’ anatarajia kuitambulisha rasmi bendi yake wiki ijayo Mei 28, mwaka huu pale Msasani Club Kinondoni, jijini Dar.
Akiongea na Mateja 20 ndani ya Triz Motel Mbezi Beach jijini Dar jana ambapo alikabidhiwa kitita cha milioni 5 kutoka kwa wadhamini wakuu wa utambulisho huo, Abama Inc, jamaa alisema ishu hiyo itakuwa ya kihistoria kwani mwanamuziki Adolf Domingeze kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) atafanya kweli.
Wasanii wengine wa Bongo watakaopoteza ile mbaya ni pamoja na Matonya, Husein Machozi, Prof Jay na wengine. Siyo shoo ya kukosa watu wangu!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment