EXTRA BONGO KUJIANDAA NA MKESHA WA MWAKA MPYA MEEDA
Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo, Ally Choki, akiimba jukwaani wakati wa onyesho lao lililofanyika Ukumbi wa San Cirro, Sinza jana. |
Kiongozi wa Wanenguaji wa Bendi hiyo, Super Nyamwela, akiwaongoza wenzake kushambulia jukwaa, wakati wa onyesho hilo. |
Rapa mahiri wa bendi hiyo, Saullo Fagason akicheza sambamba na wacheza shoo wa Bendi hiyo wakati wa shoo ya bendi hiyo kwenye Ukumbi wa Sun Cirro Sinza Dar es Salaam.
Wanenguaji wa bendi hiyo wakishambulia jukwaa.
MKURUGENZI wa Bendi ya Extra Bongo,Ally Chocky aahidi kufatoa burudani ya pekee katika Mkesha wa Chrismas,jumamosi katika Ukumbi wa Meeda jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari Chocky amesema katika shoo hiyo patakuwa na ushindani wa pekee kati ya wanamuziki na wacheza shoo ambapo Mkurugenzi mwenyewe,Ally Chocky atapanda jukwaani kuchuana na Mwalimu wa walimu,Banza Stone kwa kutoa shoo na baaada ya hapo watahamia kwa wacheza shoo wa kike ambapo Mkongwe wa Dance, Aisha Mbegu atachuana na Otilia Boniphace (Kandoro).
Murugenzi alisema, katika onyesho hilo la Mkesha wa Chrismass wataporomosha nyimbo mpya ambazo wanarekodi katika kipindi hiki pamoja na kukumbushia nyimbo zilizotamba enzi hizo kama Fadhira kwa wazazi ya Rogath hega Katapila,Mwaka wa tabu na zinginezo
Picha: Sufianimafoto Blog
0 comments:
Post a Comment