Mgeni rasmi, Waziri wa Fedha na Uchumi, Mhe. Mustafa Mkulo pamoja na Mkurugenzi wa Airtel Money, Kelvin Twisa, wakizindua huduma ya Airtel Money kutoka Airtel Tanzania, hafla hiyo imefanyika kwenye hotel ya Hyatt-Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam leo, Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania,Bw.Sam Elangallor akishuhudia tukio hilo.
Airtel Money yazinduliwa, sasa kufikisha huduma za kibenki maeneo ya vijijini kufaidisha kila Mtanzania
• Airtel Money imejipanga kutoa huduma nzuri za kibenki kupitia simu
ya mkononi katika mahitaji ya kila siku
• Yatanua wigo wa mtandao ilikuweza kutoa huduma nafuu, salama na
yenye uhakika zaidi kwa wateja
• Yaweka miundombinu bora kuwezesha kampuni zinazotoa huduma za
mahitaji ya jamii ya kila siku ikiwemo kulipa Ankara mbalimbali kwa
njia ya mtandao itakayoweza kutoa huduma kwa zaidi ya wateja milion
20
Dar es Salaam, Tanzania Desemba 7, 201
Kampuni ya simu za mkononi ya
Airtel leo imezindua upya huduma ya pesa mkononi iitwayo Airtel Money
itakayowawezesha wateja wa Airtel kufaidika na huduma za kibenki
ambazo ni nafuu, salama na zenye uhakika zaidi kwa kupitia simu zao za
mkononi. Kiwango na ubora wa huduma vitatoa fursa kwa wateja na
jamii kwa ujumla kufaidika na kukua kwa teknolojia kwa kuweza kufanya
mihamala mbalimbali kwa urahisi zaidi kupitia simu ya mkononi ya
Airtel.
Akiongea wakati wa hafla fupi ya kuzindua huduma ya Airtel Money ,
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Sam Elangalloor alisema” Huduma ya kibenki
kwa njia ya simu za mkononi itasaidia sana kuboresha maedeleo ya jamii
kwa kiwango kikubwa ikiwa tu mpangilio na ubunifu wa bidhaa
umezingatia sana maeneo muhimu ya jamii kama tulivyofanya kupitia
Airtel Money.
“Ujio Mpya wa huduma ya Airtel money itawezesha wateja kufanya baadhi
ya malipo yakibenki kupitia simu zao kama vile kulipa Ankara za huduma
mbalimabli, kuongeza muda wa maongezi pamoja na kutuma au kupokea
pesa” alisema Bw Sam.
“wakazi wengi wa vijijini wamekuwa wakikosa huduma kama hizi za
kibenki kutokana kushindwa kumudu gharama inayotokana na umbali wa
kufata huduma hizo mbali na vjiji vijiji vyao, lakini kwa kupitia
huduma ya Airtel Money wateja wote wenye maeneo ya mjini na vijijini
sasa wataweza kupata huduma za kifedha nafuu na za kisasa kwa kutumia
mtandao wa Airtel ulioenea nchini kote .
Mtandao mpana tulionao Airtel katika maeneo ya vijijini unaenda
sambamba na kuwa na Wakala wengi watakaotoa huduma ya Airtel Money ili
kuendelea kuunganisha maeneo muhimu yatakayofaidisha watumiaji na
kutoa huduma za kisasa zaidi ikiwa ni pamoja na kuunganisha ulipaji wa
Ankara mbalimbali za mashirika na taasisi muhimu zinazoendana na mfumo
huu wa kibenki kupitia mtandao
Kwa upande wake waziri wa fedha na uchumi, Mh Mustafa Mkulo
aliwapongeza Airtel Tanzania kwa kushirikiana na serikali katika
kupenyeza huduma za kibenki kwa kupitia simu ya mkononi ili kusaidia
kuinua uchumi. Alisema nimefarijika sana kuona huduma za simu
zinafanya baadhi ya huduma zilizo sambamba na zile za benki. Hii ni
moja ya mikakati ya kuendeleza huduma za kibenki ambayo serikali yetu
ilijiwekea miaka miwili iliyopita
Aliongeza” kwa kupitia mtandao wa Airtel ulioenea zaidi hasa vijijini
kutawezesha idadi kubwa ya wakazi wa vijijini kujikita kwenye shughuli
za biashara wakati ambapo tunaendelea kufikia malengo tuliojiwekea
katika hadi ifikapo mwaka 2025. Tunaamini Airtel money itakuwa
chachu ya kusaidia shughuli za kiuchumi kama vile kilimo, madini,
uvuvi na matokeo yake kwa jumla ni kuchangia katika kukua kwa uchumi
wa nchi yetu.
Naye waziri wa Sayansi na Teknologia Mh. Makame Mbarawa aliongeza “Ni
dhahiri kabisa kukua kwa sekta ya mawasiliano katika nchi yetu
yameleta chachu kwa maendeleo ya wakulima,wavuvi, wachimba madini na
wafanyabiashara mbalimbali kuweza kuwasiliana na kufanya shughuli za
uzalishaji kwa ufanisi Zaidi.Taasisi za kifedha na kibenki yanaweza
kua hayajawafikia watanzania kwa kiasi kikubwa.Changamoto kwao sasa
ni kuweza kufanya kazi kwa pamoja kama washirika katika maendeleo na
makampuni ya simu kupitia huduma mbalimbali kama Airtel money ili
kukabiliana na mabadiliko ya teknolojia yanayoenda kwa kasi na
hatimaye kusaidia watanzania kwa ujumla.
Sisi kama wizara tunaahidi kushirikiana na makampuni mbalimbali ya
simu ikiwemo Airtel pamoja na mitandao kwa ujumla kuhakikisha Tanzania
inakua moja kati ya nchi inayotoa huduma madhubuti na za kisasa Zaidi.
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa kitengo cha Airtel Money Bw. Kelvin
Twissa alisema “ huduma ya Airtel Money itapatikana kwa wateja wote
wa malipo ya kabla na baada na kujiunga na huduma hii ni bure katika
vituo vyetu vyote vya Airtel na mawakala wote walioenea nchi nzima.
Wakala wa Airtel Money waliosambaa nchi nzima watawawezesha wateja
kufanya miamala ya pesa popote walipo. Mara mteja atakapoweka pesa
kwenye akaunti yake ya Airtel Money ataweza kutuma hela, kununua muda
wa maongezi au kulipia ankara za mahitaji mbalimbali ya kila siku
wakati wowote au kufanya manunuzi bila usumbufu kwa urahisi mahali
popote nchini.
Airtel tumejipanga kuhakikisha tunafikia malengo ya Milenia ya kuondoa
umasikini na kuongeza Mapato ya taifa ya ndani kwa ujumla (GDP) kwa
kushirikiana na wadau wa sekta mbalimbali kama kilimo na huduma za
fedha zikiwepo taasisi ndogondogo za fedha, Ushirikiano wetu uliopo
tangu awali kati yetu na shirika la tumbaku katika kusimamia taarifa
za msimu mbalimbali kwa wakulima sasa tutaliunganisha na hili la
huduma za kibenki kupitia Simu ya mkononi kusaidia kuongeza tija zaidi
kwa wakulima katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania” alisemaTwissa
0 comments:
Post a Comment