Picha ya mele ya Spice, inayodaiwa kuzama ikiwa imeegeshwa bandarili siku za nyumba kabla ya kukumbwa na masahibu hayo
TAARIFA nilizopata hivi punde zinasema kwamba watu takribani 2,000 wanahofiwa kupoteza maisha yao baada ya Meli ya Spice, kuzama ikitokea Unguja kuelekea Pemba, ilipofika kwenye mkondo wa Nungwi.
Chanzo chetu kinasema kuwa hadi sasa ripoti hii haijawa sahihi maana hakuna yoyote aliyetoa majibu na uhakika kamili ya idadi ya watu waliyopoteza maisha hata waliyookolewa kwenye ajali hiyo.
Hatuna taarifa kamili ila serikali itakapotamka lolote juu ya idadi hii tutawafahamisha zaidi.
Chanzo chetu kilichoshuhudia tukio hilo kilisema kwamba Meli hiyo ilianza kuzama kiubavu na imechukua muda kuzama hadi kuishia majini im echukua muda mrefu sana.
Kwa mjibu wa ripoti mbalimbali za redio (ISTIQAMA) za hapa nchini inadaiwa kuwa sababu kubwa iliyoifanya meli hiyo izame ni wingi wa mizigo na abiria kuzidisha idadi yake ya kawaida.
Chanzo chetu kiliendelea kuronga kwamba abiria wengi waliyokuwemo kwenye meli hiyo walikuwa ni wazazi na watoto wao waliyokuwa wameenda visiwani Pemba kwaajili ya kusherehekea sikukuu ya Idd na hapo walikuwa wakilejea kwaajili ya kuwahi masomo.
TAARIFA DAKIKA MBILI ZILIZOPITA KUTOKA CLOUDS REDIO, KWA MJIBU WA DJ FETTY, INASEMEKANA HADI SASA WATU ZAIDI YA 250 WAMESHAOKOLEWA
Saturday, September 10, 2011
Labels:
www.mateja20.blogspot.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment