Social Icons

Tuesday, August 16, 2011

WASHINDI WA SHINDANO LA TUSKER MILIONI 500 KWA MASHABIKI WATEMBELEA KIWANDA CHA SERENGETI


Mpishi msaidizi wa kiwanda hicho, Bwana Donan Ritte akionyesha mtambo unaosafisha maji taka yaliyotumika kiwandani hapo kwa ajili ya kutunza mazingira.


Mpishi msaidizi wa Serengeti Breweries Donan Ritte akifafanua jambo mbele ya washindi wa promosheni ya shindano la Tusker milioni 500, kwa mashabiki jinsi chupa zinavyosafishwa kabla ya kuwekwa kimimika chochote.
Donan Ritte akiwaonesha washindi mbalimbali walioshinda zawadi katika promosheni ya shindano la Tusker milioni 500 kwa mashabiki lililomalizika hivi karibuni,moja ya mitambo inavyofanya kazi.
Meneja Usalama wa kampuni ya bia ya Serengeti John Nyamwanga Mataria (katikati), akitoa maelekezo kuhusiana na kitengo chake cha mambo ya usalama kazini kwa washindi hao leo, ambapo wametembelea kiwanda cha Serengeti Breweriers kilichopo Chang'ombe Temeke jijini Dar , na kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji wa bia na vinywaji vingine katika kiwanda hicho, kulia kwake ni meneja wa bia ya Tusker Ritha Mchaki.

Donan Ritte akionyesha kinu ambacho hupokea ngano kabla ya kwenda kukobolewa, tayari kwa kusagwa na kupikwa katika mitambo ya kiwanda hicho, kulia ni Meneja wa kinywaji cha Tusker,Rittah Mchaki akisikiliza kwa makini.
Donan Ritte, akionyesha moja ya kifaa maalum kinachoonyesha namna ngano inavyokobolewa tayari kwa kufuata hatua nyingine kwa washindi hao.
Baadhi ya washindi ,wakisalimiana na Meneja wa kiwanda hicho Bwa.Colman Hanna.

0 comments: