Social Icons

Monday, August 1, 2011

VODACOM YAJA KIVINGINE NA HUDUMA YA M-PESA

"NA HII IGENI SASA', Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Bi. Mwamvita Makamba wanne kutoka (kushoto) na Mkuu wa kitengo cha huduma za kifedha wa kampuni hiyo Bw. Jacques Voogt kushoto kwake, wakishikana mikono kuashiria uzinduzi rasmi wa muonekano mpya wa huduma ya Vodacom M-PESA kwa wateja wake wote nchini ambayo inaendana sambamba na kauli mbiu ya "Kazi ni Kwako" kwa kuihusisha huduma hiyo na kazi anazozifanya 'Superman' za uharaka, usalama, uhakika na utayari wake wa kusaidia jamii wakati wowote ule na mahali popote pale.
Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Bi. Mwamvita Makamba akimsikiliza kwa umakini, Mkuu wa Kitengo cha huduma za kifedha wa Vodacom Tanzania Jacques Voogt, akiongea wakati wa uzinduzi rasmi wa muonekano mpya wa huduma ya Vodacom m-pesa kwa wateja wake wote nchini ambayo inaendana sambamba na kauli mbiu ya "Kazi ni Kwako" kwa kuihusisha huduma hiyo na kazi anazozifanya 'Superman' za uharaka, usalama, uhakika na utayari wake wa kusaidia jamii wakati wowote ule na mahali
Baadhi ya watu waliohudhuria hafla hiyo ya uzinduzi wa huduma hiyo.
Baadhi ya wapiga pcha za magazeti mbalimbali wakiwa bize katika kunasa matukio ya uzinduzi wa hudunhiyo.


Wafanyakazi mbalimbali wa Vodacom Tanzania wakiwa kwenye mfano wa vazi analovaa"Superman" wakati wa uzinduzi rasmi wa muonekano mpya wa huduma ya Vodacom m-pesa kwa wateja wake wote nchini ambayo inaendana sambamba na kauli mbiu ya "Kazi ni Kwako" kwa kuihusisha huduma hiyo na kazi anazozifanya 'Superman' za uharaka, usalama, uhakika na utayari wake wa kusaidia jamii wakati wowote ule na mahali popote pale.


VODACOM Kazi ni kwako!

UFUNGUZI WA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM MJINI DODOMA

Mwenyekiti wa CCM taifa, Jakaya Kikwete, Makamu Mwenyekiti CCM Zanzibar, Aman Abeid Karume (wa tatu kushoto), Rais wa Zanzibar, Dkt Ali Mohamed Shein na Mwenyekiti wa CCM Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi (kushoto), Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Pius Msekwa (kulia) na Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Willson Mukama, wakiwa katika ufunguzi wa Kikao cha Kamati kuu kilichofunguliwa leo, katika Ukumbi wa CCM Makao Makuu mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, akiingia katika Ukumbi wa CCM Makao Makuu mjini Dodoma, leo Julai 31, wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Kamati kuu. Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Willson Mukama.
Wajumbe, Abdulrahman Kinana Mjumbe wa Kamati Kuu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Samia Hassan Suluhu (katikati) na Nape Nnauye, wakiwa ukumbini humo.
Wajumbe, Waziri wa Ulinzi, Hussein Mwinyi (katikati) Stephen Wasila (kulia) na Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa.
Wajumbe, Waziri wa Mambo ya Ndani Shamsi Vuai Nahodha na Spika wa Bunge, Anne Makinda, wakiwa ukumbini humo.


PICHA: SUFIANIMAFOTO.BLOGSPOT

0 comments: