VODACOM MISS SPORTS LADY 2011 NI LOVENESS
Vodacom Miss Sports Lady 2011, Loveness Flavian akiwa katika pozi la ukweli baada ya kushinda na kutangazwa kutwaa taji hilo na kuwa mrembo wa tatu kati ya warembo 15 waliojikatia tiketi ya kutinga katika Nusu fainali za Vodacom Miss Tanzania 2011, zinazotarajia kufanyika Septemba 10, mwaka huu jijini Dar es Salaam. Vodacom Miss Top Model, Mwajabu Juma (katikati) ambaye alikuwa mrembo wa kwanza kuingia hatua ya Nusu Fainali ya Vodacom Miss Tanzania 2011 akiwa na mrembo wa pili kuingia katika hatua hiyo ya 15 bora Vodacom Miss Photogenic Tracy Mabula (kushoto) wakipozi kwa picha na mwenzao wa tatu kutinga katika hatua hiyo baada ya kutwaa taji la Vodacom Miss Sports Lady, Loveness Flavian, usiku wa kuamkia jana katika Jumba la Vodacom Dar es Salaam. Warembo waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora ya Vodacom Miss Sports Lady wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kutangzwa mshindi usiku wa kuamkia jana. Kutoka kushoto ni Rose Hurbert, Husna Maulid, Loveness Flavian, Salha Izrael na Delillah Ghalib. Mchujo waa warembo hawa ulifanyika katika siku ya michezo ya Vodacom Miss Tanzania wiki iliyopita.Vodacom Miss Sports Lady, Loveness Flavian, akipongezwa na warembo wenzake wa Vodacom Miss Tanzania waliofanikiwa kuingia tano bora ya kuwania taji hilo la michezo baada ya mwenzao huyo kutajwa kuwa ndiye mshindi na anakuwa mrembo wa tatu kuingia katika hatua ya Nusu fainali za Vodacom Miss Tanzania mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment