


KAMPUNI ya simu ya mkononi ya Airtel leo imeeleze mpango wake wakugawa jessy na vyeti kwa timu zote zilizoshirika katika mashindano ya Airtel Rising Star mashindano ya yanayoshirikisha jumla ya shule za sekondari 24 kutoka mikoa ya Iringa, Mwanza, Dar es salaam na Morogoro kwa wachezaji wa umri wa chini ya miaka 17.
Mashindano ya Airtel Rising Star yalianza mwenzi Julai mwaka huu na yataendelea kwa timu zilizoibuka washindi hadi Desemba mwaka huu
Akizungumza na waandishi wa habari Jackson Mmbando Meneja Uhusiano wa Airtel alisema, mashindano ya Airtel Rising star yalizinduliwa rasmi kwa kushirikiana na Manchester united kwa lengo la kuinua vipaji vya vijana walio chini ya umri wa kumi na saba, na leo tunatangaza dhamira yetu yakuendelea kuboresha shule zilizoshriki ili mwaka kesho yatakapokuwa yanaendelea yaweze kuleta muamko zaidi kwa vijana
Kesho ijumaa tunaanza kugawa jezi mikoani na tutaanza na Morogoro kisha Iringa 31/8/2011 na mwanza 2/9/2011
Shule ambazo tayari zimeshafaidika na mpango huu wa jezi za Rasing star mkoa ni Jitegemee Secondari, Kinyelezi Secondari, Azania Secondari,Makongo Secondari, Temeke Secondari, Twiga Secondari, Mbande Secondari, Msongola Secondari, Mpigimagohe Secondari, Kibugumo Secondari, Misitu Secondari, Goba Secondari
Mashindano ya Artel; Rising Star yataendelea baada ya ramadhani ambapo yatahusisha timu moja kutoka katika kila mkoa ambapo DSM utawakilishwa na jitegemee secondari, Morogoro -Mwembesongo Secondari, Iringa Tagamenda Secondari, Mwanza Taqwa Secondari
Sambamba na hili mashindano haya yatatuwezesha kupata wacheza 6 nyota ambao watajiunga na Airtel cliniki kwa mafunzo zaidi yatakayo tolewa na walimu kutoka Manchester united.
Ili kuhamasisha vijana kufanya vizuri zaidi mbali na wale wachezaji 6 wanaoingia kwenye klinic ya Manchester United airtel Tumejipanga kutoa zawadi kwa mchezaji mwenye nidhamu, golikipa bora, Timu itakayotwaa ubingwa wa kwanza na mshindi wapili ambapo zawadi zao tutaziweka wazi baada ya mfungo wa ramadhan pia.
Aidha Meneja huduma kwa jamii wa Airtel Tunu Towo Kavishe pia alieleza “mbali na michezo Airtel inatoa misaada mbalimbali kwa jamii hususani katika swala la elimu, kwa kupitia mpango maalumu ujulikanayo kama shule yetu na kuweza kugawa vitabu kwa shule za sekondari zaidi ya 800 zenye thamani ya shilling billion moja, tunaahidi kuendelea kushirikiana na wizara ya elimu katika kuchangi na sekta ya elimu nchini pamoja na kuinu michezo kuanzia sheleni.
Kesho tutakuwa morogoro na kutoa vitabu kwa shule ya Sua Sekondari vyenye thamani shilingi milioni moja. Pia tutatemelea shule zilizoshiriki Airtel rising star na kuwapatia vifaa vya michezo ili waendeleea kujiandaa na mashindano ya airtel Rising star ya mwakani.
0 comments:
Post a Comment