Asha Baraka akiongea jambo mbele ya waandishi wa habari.
Baadhi ya waandiishi wa habari wakishuhudia duka hilo.
DUKA la vipodozi linalotarajiwa kutolewa zawadi kwa Kimwana wa Twanga Pepeta 2011, limetambulishwa rasmi leo mbele ya waandishi wa habari, maeneo ya Kinondoni Studio, jijini Dar es Salaam, karibu na duka la Wasafi Classic.
Akiongea kwenye mkutano wa waandishi wa habari, mkurugenzi wa mashindano hayo, Asha Baraka, alisema kwamba wameona ni vyema kuziweka wazi zawadi za washindi wa shindano hilo ili kuepusha utata wa aina yoyote.
Alisema zawadi zingine zitakazotolewa siku hiyo ni pamoja na Shilingi 500,000 kwa mshindi wa pili, Sh. 300,000 kwa mshindi wa tatu na washiriki wengine watapata kifuta jasho cha Shilingi 100,000 kila mmoja.
Mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika Julai 8 mwaka huu ndani ya ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment