Picha ya kwanza juu Miss Chang’ombe 2011, Cynthia Kimasha, akiwapungia mkono mashabiki wake muda mfupi baada ya kutwaa taji hilo. Picha ya pili juu Miss Chang’ombe 2010, ambaye pia ni Miss Tanzania mwaka 2010/2011, Genevieve Emmanuel Mpangala, akiwaaga mashabiki wake kwa kupunga mkono muda mfupi kabla ya kukabidhi taji hilo.
KATIKA kinyang’anyiro cha kumsaka mlimbwende wa kitongoji cha Miss Chang’ombe 2011/12 usiku wa kuamkia leo, Cynthia Kimasha amewabwaga warembo wengine 12 na kulitwaa taji la kitongoji hicho. Tukio hilo lilifanyika Temeke ndani ya ukumbi wa TCC Club, Changombe jijini Dar es Salaam, likisindikizwa na bendi ya Mapacha Watatu, na mashabiki kibao kutoka pande mbalimbali.
Genevieve (kulia) akimkabidhi taji Cynthia Kimasha mara baada ya kutangazwa mshindi.
Cynthia (katikati), akiwa kwenye pozi na mshindi wa pili Husna Twalib (kushoto), na mshindi wa tatu Joyce Mawenda baada ya kuibuka kidedea.
Baadhi ya mapaparazi na mashabiki wa shindano hilo wakichukua picha za kumbukumbu kwenye kinyang’anyiro hicho.
Baadhi ya wadhamini wa shindano hilo wakifuatilia mchakato mzima ulivyokuwa.
Mashabiki waliojitokeza kwenye mchakato huo wakifuatilia kwa furaha tele zoezi hilo.
Mwanamuziki wa Mapacha Watatu, Khaleed Chuma ‘Chokoraa’ (katikati), akiongoza safu ya wanenguaji wake kusherehesha mashindano hayo.
0 comments:
Post a Comment