Social Icons

Saturday, April 2, 2011

WALEMAVU WA NGOZI WAPEWA MSAADA

Mwenyekiti wa Chama cha Maalbino Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, Seif Ulate akimkaribisha Miss Pogress 2010 kwa ajili ya kuzungumza na watu waliohudhuria.

Miss Progress International 2010 ambaye pia alishinda taji la Miss Tanzania 2009, Julieth William jana alitoa msaada wa shilingi milioni moja na laki nne kwa wanafunzi 30 ambao ni walemavu wa ngozi wa shule za msingi za Wilaya ya Ilala kwa ajili ya kushonewa sare za shule.

Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo katika Ukumbi wa Heros Inn uliopo Ilala jijini Dar es Salaam, Julieth alisema kuwa ametoa msaada huo ukiwa ni sehemu ya mradi wake wa kusaidia walemavu wa ngozi hususan watoto ili waweze kupata elimu bora na watimize malengo yao kama watu wa kawaida.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa chama cha maalbino wilaya ya Ilala, Seif Ulate amemshukuru Julieth kwa msaada huo na kumtaka aendelee na moyo huo wa kusaidia kwani wataweza kuwashonea sare za shule ambazo ni mashati ya mikono mirefu na suruali ili wasome kwa raha kama watoto wengine.

Julieth akizungumza na walengwa.

Watoto na wazazi waliohudhuria wakimsikiliza Julieth wakati akitoa ufafanuzi wa msaada huo.

Miss Julieth (kulia) akikabidhi fedha hizo kwa mtoto Maria Laurian.

Bi. Rachel Katemi aliyehudhuria kwa niaba ya Afisa Ustawi wa jamii wilaya ya Ilala akimshukuru Julieth kwa msaada alioutoa.

0 comments: