Social Icons

Thursday, April 14, 2011

UGALI NA SAMAKI WA THE ATRIUMS HOTEL DUDE ASHINDWA KUINUKA

Kulwa Kikumba ‘Dude’ (kulia) akipata msosi na shabiki wake Ashura Malekela katika Hotel ya kifahari ya The Atriums iliyopo Sinza Afrikasana jijini Dar es Salaam wiki iliyopita.

MUHUSIKA katika kipindi cha Bongo Dar es Salaam ambacho kilikuwa kikirushwa katika Runinga ya Tbc1, Kulwa Kikumba ‘Dude’ Ijumaa ya wiki iliyopita alijiachia katika Hotel ya kifahari ya The Atriums iliyopo Sinza Afrikasana jijini Dar, akiwa na shabiki wake Ashura Malekela wa Kinondoni jijini Dar.

Dude aliagiza ugali na samaki mkubwa aina ya sato ambapo mwishowe alishindwa kuinuka baada ya kuonekana kuvimbiwa.

“Unajua nilipoagiza huu ugali na samaki nilijua ni kama ninavyoagiza nikiwa nyumbani kwangu, kumbe nimejiingiza ‘choo cha kike’ nilivyoletewa samaki mkubwa ili nisionekane nimechemsha nikataka kuhakikisha nammaliza wote, matokeo yake ndiyo haya,” alisema Dude.

Fulu kujiachia kwa Dude kulitokana na zoezi zima la Jiachie na Staa wako linaloendeshwa na gazeti hili la kijanja na kudhaminiwa na hotel hiyo ya mastaa.

Dude na Ashura walifurahia huduma pamoja na mandhari nzuri ya hotelini hapo hadi kufikia muigizaji huyo kufikia kuwa na wakati mgumu baada ya kukandamiza msosi ambao alidhani anawakomoa waandaaji.

0 comments: