WASHIRIKI wa kinyang'anyiro cha kumsaka Miss Dar City Center 2011, wanazidi kubanana mbavu katika kambi yao iliyopo Lamada Hotel Ilala jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Mateja20 mapema leo, Mkurugenzi wa kampuni ya Fetty Entertaiment, ambayo inaratibu shindano hilo kwa mwaka huu, Fatma a.k.a Fetty alisema kumba, kutokana na wingi wa warembo alionao ni zahili kabisa kwa sasa wanabanana mbavu ili kuhakikisha kila mmoja anajiweka sawa katika mazoezi kutokana na wengi wao wanasifa za kushinda.
Fetty aliongeza kuwa, tangu ajiingize kwenye mambo ya urembo hakuwahi kuona kambi inakuwa na walimbwende wenye sifa za kunayakuwa taji wengi kama ilivyo kwenye kambi hiyo.
" Kusema kweli katika maisha yangu yote hasa tangu nilipojiingiza kwenye maswala haya ya walimbwende sikuwahi kuona kambi ikiwa na warembo wengi kama hawa wenye vigezo vya kushinda"
Hivyo Fetty alisema kwamba, kutokana na hari hii mwaka huu patachimbika kwa majaji kumpata atakae chukua taji hili.

0 comments:
Post a Comment