Habari za kusikitsiha zilizotufikia asubuhi ya leo zinasema kuwa Mzee Hammie Rajab (kwenye kiduara) amefariki dunia katika hospitali ya Amana jijini Dar es salaam alfajiri ya leo, ambako alikuwa amelazwa kutokana na ugonjwa wa malaria. Mzee Hammie, alikuwa ni movie Director, Script writer na mtunzi wa hadithi za vitabu maarufu nchini Tanzania. Moja ya kazi zake maarufu kwa upande wa filamu ni movie ya Tears On Valentine Day, ambayo iko sokoni hivi sasa. Pichani, juu na chini, akiwa kazini aki direct movie hiyo siku za hivi karibuni. Habari zaidi zitawajia baadae.
Hapa akiwa na mmoja wa mastaa wa filamu hiyo, Vannelies Evans 'joanita' ambaye kwa sasa yuko masomoni nchini Marekani. Chini ni kipande cha 'Behind the scene' ya filamu hiyo akiwemo Hammie rajab kazini. YEYE NI WA MWENYEEZI MUNGU, NASI PIA NI WA MWENYEEZI MUNGU NA KWAKE SOTE TUTAREJEA. MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI - AMIN
0 comments:
Post a Comment