Khadija Mnoga Kimobitel akijielezea mara baada ya kutangazwa.
MKURUGENZI wa kampuni ya African Stars Entertaiment (Aset), Asha Baraka, leo amemtambulisha rasmi kwa waandishi wa habari mwanamuziki Khadija Mnoga (Kimobitel) ambaye ameamua kurejea katika bendi yake ya Twanga Pepeta.
Akizungumza katika ofisi za Aset zilizoko Kinondoni, jijini Dar es Salaam mara baada ya kumtambulisha msanii huyo aliyetokea bendi ya Extra Bongo, Baraka alisema kuwa Kimobitel ameamua kuejea katika bendi hiyo baada ya kuchoka na kile alichokiita “ubabaishaji” katika bendi hiyo ya awali iliyo chini ya mwanamuziki Ally Choki.
“Nimeamua kurudi nyumbani kwani sikufukuzwa na mtu yeyote ndani ya Twanga Pepeta. Niliamua tu kupumzika. Mbaya zaidi, kule nilipotoka kumezidi sana tabia za ubabaishaji,” alisema Mnoga.
Wakati huohuo, Asha Baraka amewatambulisha waimbaji wengine na uongozi mpya wa bendi hiyo tangu kifo Abuu Semhando, aliyekuwa meneja wa bendi hiyo.
Asha Baraka akisisitiza jambo mara baada ya kumtangaza Kimobitel.
Haji Ramadhani aliyetokea Bongo Star Search (BSS) (mwenye fulana nyekundu) akitambulishwa mbele ya wanahabari.
Mwimbaji mwengine aliyejiunga na Twanga Pepeta akitokea Bagamoyo Sound, Venance Joseph, akiwa katika pozi mara baada ya kutambulishwa.
0 comments:
Post a Comment