AJALI iliyoyahusisha magari matatu imetokea tena jana jioni eneo la Msamvu barabara ya Korogwe na kusababisha gari ndogo kuharibika vibaya kufuatia gari hilo kugongwa na magari mawili upande wa mbele na ule wa nyuma.
Kwa mujibu wa watu walishushuhudia tukio hilo waliueleza mtandao huu kwamba, Fusso lililokuwa limebeba mzigo wa kuni liliharibika ghafla eneo la mlima, jirani na Shule ya Msingi Msamvu,na wakati 'Tingo' wa Fusso hilo akijiandaa kuweka magogo kwenye mataili, lori hilo lilirudi nyuma na kuligonga gari dogo lililokuwa nyuma yake ambalo nalo liligogwa kwa nyuma na Hiace iliyokuwa nyuma yake.
Hivi juzi katika barabara hiyo hiyo, eneo la Masika kulitokea ajali iliyoyahusisha magari matatu na pikipiki moja. Hivyo Mtandao huu unawahasa madereva wote kuwa makini wanapokuwa katika barabara hii.
Picha zifuatazo zinaonesha tukio hilo lilivyokuwa:

0 comments:
Post a Comment