Social Icons

Thursday, February 24, 2011


Meneja masoko wa Airtel, Kelvin Twissa akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari.
Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Airtel, leo imetangaza huduma yake mpya itakayofahamika kwa jina la Airtel Flava.

Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya kampuni hiyo yaliyopo Kinondoni Moroco jijini Dar es Salaam, meneja masoko wa Airtel Kelvin Twissa alisema kwamba, huduma hiyo itakuwa mahususi kwa kuchangamsha huduma za wateja wao.

Twissa alisema kuwa, kupitia huduma hiyo wateja wote wa Airtel wataweza kujichagulia muziki wowote na kuusikiliza kupitia simu zao wakati wowote kwa kupiga namba 15565 na kuchagua muziki husika.



Baadhi ya waandishi wa habari wakinakili baadhi ya maelezo kutoka kwa meneja huyo.


Meneja wa huduma za ziada wa Airtel, Frank Semaganga akifafanua namna ya kuitumia huduma hiyo.
Polisi mkoani Mwanza wameridhia maandamano yaliyoandaliwa na Chadema, kupinga malipo ya fidia kwa Kampuni ya Dowans, kuongezeka kwa gharama za maisha na kupanda kwa gharama za umeme.

Katibu wa Chadema Mkoa wa Mwanza, Wilson Mushumbusi alisema tayari wamekwishakamilisha maandalizi ya maandamano hayo, yatakayofanyika leo kuanzia saa 8: 00 mchana na kufuatiwa na mkutano wa hadhara.

Maandamano ya Mwanza yanafanyika takriban miezi miwili tangu kutokee mauaji ya raia waliopigwa risasi na polisi mkoani Arusha, wakati walipokuwa wakizuia maandamano ya Chadema mkoani humo.

Katika tukio hilo la Januari 6, mwaka huu watu kadhaa walijeruhiwa, polisi wa Arusha walimwaga damu za watu kadhaa, walioshiriki na wasioshiriki maandamano yaliyoandaliwa na Chadema.

Risasi za moto na mabomu ya machozi vilitumika katika jitihada za polisi kuzima maandamano ya Chadema, wakitekeleza amri ya Mkuu wa Jeshi hilo, Ispekta Jenerali Said Mwema ambaye awali aliyapiga marufuku baada ya kuwa yameruhisiwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye.

Jana Mushumbusi alisema maandamano ya Mwanza yatahitimishwa kwa mkutano wa hadhara utakaofanyika katika Viwanja vya Furahisha, Kirumba jijini hapa kuanzia saa10:00 jioni.

Tayari Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amewasili jijini hapa kwa lengo la kushiriki maandamano hayo ya kwanza kufanyika Mwanza tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani, Oktoba 31 mwaka jana.

Dk Slaa aliwasili jijini Mwanza jana mchana. Viongozi wengine wa Chadema wanaotarajiwa kushiriki maandamano na baadaye mkutano ni Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe.

Mushumbusi alisema mbali na viongozi wa taifa wa Chadema, wabunge wote wa chama hicho wanatarajiwa kuhudhuria maandamano hayo.

Aliwataka wapenzi, wanachama na Watanzania wote kwa ujumla wanaochukia ufisadi kutoka wilaya mbalimbali za Mkoa wa Mwanza kushiriki.

“Sisi maandalizi yetu yamekamilika na viongozi wote wa kitaifa wa chama na wabunge wote wa Chadema wamethibitisha kuhudhuria maandamano yetu ambayo yataanzia Kituo cha Mabasi cha Buzuruga, Nyakato na kupita Barabara ya Mwanza-Musoma, Nyerere, Kenyatta na kuingia Barabara ya Uwanja wa Ndege kwenda hadi katika Viwanja vya Furahisha,” alifafanua katibu huyo wa Chadema.

Mushumbusi alisema kutokana na wao kufanya maandamano ya amani, chama chake kimeandika barua ya taarifa kwa Jeshi la Polisi na kuzingatia sheria ya kutoa taarifa kwa jeshi hilo saa 48 kabla ya kuandamana na wala siyo kuomba kibali.

“Barua ya kuwataarifu Jeshi la Polisi kuhusiana na maandamano tuliwakabidhi tangu Februari 20, mwaka huu na Jeshi la Polisi limekubaliana na maandamano yetu na njia ambazo tutapitia, hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi, tutaendelea na maandamano yetu kama yalivyopangwa,” alieleza Mshumbisi.

Katibu huyo alisema lengo la maandamano yao ni kupinga vitendo vya ufisadi, malipo ya Sh94 bilioni ya tozo kwa ajili ya kampuni ya Dowans, kupinga kupanda na kuongezeka kwa bei ya umeme nchini na kuongezeka kwa gharama za maisha.

Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Simon Sirro alipoulizwa kuhusu maandamano hayo, alisema jeshi lake limejipanga na kusema hawana tatizo na maandamano hayo na kwamba watahakikisha wanatoa ulinzi mkali kulinda watu wasio na nia njema kutumia mwanya huo kuzusha vurugu.

“Hatuna tatizo na maandamano, haya tumeridhia na kukubaliana ni wapi watapita, tumejipanga kwa ulinzi ili kuhakikisha maandamano hayo yanakuwa ya amani na salama kwa watu wengine na mali zao,” alieleza Kamanda Sirro.

Wachunguzi wa mambo waliozungumzia maandamano hayo walisema huenda yakapata ushiriki wa watu wengi kutoka na mada ziliyopangwa kuzungumzwa, kuwagusa watu wengi.

CHANZO: MWANANCHI

George Kavishe, akiongea jambo katika hafla hiyo.
SEMINA ya Wateule wa Tuzo za Kili Music Awards 2011 jana ilifana katika ukumbi wa Paradise Hotel, jijini Dar es Salaam, ambapo wasanii hao walikutana na uongozi mzima ulioandaa shughuli hiyo na kubadilishana mawazo.

Akiongea na wateule hao, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe, alisema amelazimika kuwaalika mapema wateule hao ili kuchanganua baadhi ya makundi (category) yaliyopangwa kimakosa ili kuzuia malalamiko kutoka kwa washiriki.


Aidha mratibu wa tuzo hizo kutoka Baraza la Sanaa Tanzania (Basata), Angelo Luhala, alisema wito huo wa wasanii ni njia moja ya kuwapa fursa ya kupendekeza marekebisho kabla ya siku ya utoaji tuzo hizo.


Angelo Luhala, akizungumza na wasanii wa semina hiyo.

Msanii wa kundi la Orijino Komedi, Sylvester Mujuni ‘Mpoki’ (kulia), akibadilishana mawazo na msanii wa ‘Hip Hop’, Joh Makini, kwenye hafla hiyo.


Msanii wa mashairi, Mrisho Mpoto (kulia), na msanii mwenzake, Kassim Mganga, wakifuatilia baadhi ya makundi kama yalivyoandikwa.

Mkurugenzi wa Jahazi Modern Taarab, Mzee Yusuf, akipata matunda muda mfupi kabla ya kuingia kwenye kikao hicho.

Msanii wa Hip Hop, Faridy Kubanda (Fid Q) akihoji jambo fulani katika hafla hiyo.

Ali Kiba naye hakuwa nyuma kuuliza swali kwenye kikao hicho.

Kiongozi wa bendi ya African Stars International (Twanga Pepeta) Luiza Mbutu (katikati), akiwa kwenye picha na baadhi ya wanamuziki waliyojiengua kwenye bendi hiyo ambao ni Kalala Junior (kulia), na Khaleed Chuma ‘Chokoraa’ (kushoto), nyuma yao (kulia), ni Rapa wa Twanga Pepeta, Said Msafiri Sayai (Msafiri Diouf) na Meneja wa bendi ya Mapacha Watatu, Hamisi Dakota.

Baadhi ya wasanii waliohudhuria mchakato huo wakifuatilia zoezi hilo kwa ujumla.

Mzee Yusuf (kushoto), akiwa na Kassim Mganga ambaye ameshikilia magongo yake.

"SAIDIA GONGO LA MBOTO"


Tunapenda kuwakumbusha tena wakazi wote wa UK kuwa kutakuwa na harambee ya Kuchangia Wahangwa wa GONGO LA MBOTO nyumbani Tanzania. Hivyo basi tunawaomba wote mjitokeze kwa wingi ili tuweze kufanikisha zoezi hili. Kwa maelezo zaidi angalia video fupi kutoka kwa Mama Balozi Mrs Joyce Kallaghe na pia unaweza kupata anuani na mda wa
kufika.

KWA WAKAZI WA LONDON NA MIJI YA KARIBU AU KAMA UTA WEZA KUFIKA TUTAKUWA:

AFRICAN VILLAGE BAR & RESTAURANT
81 BROAD LANE
SEVEN SISTERS
LONDON

NW15 4DW

SIKU: JUMAPILI TAREHE 27 FEB 2011

MUDA: 3PM - LATE

KWA WAKAZI WA READING NA MIJI YA KARIBU AU KAMA UTA WEZA KUFIKA TUTAKUWA:
VINCENT RESTAURANT
288-290
OXFORD ROAD
READING

SIKU: JUMAMOSI 26 FEBRUARY 2011

MUDA: 3PM - LATE

TAFADHALI LETA CHOCHOTE ULICHO NACHO ILI TUWEZE KUWASAIDIA HAWA NDUGU ZETU WALIO PATWA NA MAAFA HUKO NYUMBANI TANZANIA

KWA WAKAZI WA MIJI MINGINE AMBAO MTASHINDWA KUFIKA LONDON TUNAPANGA UTARATIBU WA JINISI GANI TUNAWEZA KUFIKA KATIKA MIJI YENU KUKUSANYA HIYO MISAADA. TUTAWAJULISHA MARA MIPANGO HII ITAKAPO KAMILIKA.

AU KAMA UNA CHOCHOTE UNAWEZA PIA UKAWEKA KWENYE ACCOUNT IFUATAYO NA TUNAOMBA UANDIKE JINA LAKO AS REFERENCE ILI TUJUE PESA IMETOKA KWA NANI AND CAN BE ACCOUNTED FOR!!


BANK: BARCLAYS
NAME: MISS SHILLA GABRIEL FRISCH
ACCOUNT NUMBER: 40974382
SORT CODE: 202941



FOR MORE INFORMATION YOU CAN REACH US ON


+447527190239,
+447404332910,
+447876126862,
+4407747129987,
+447944473389


TAFADHALI MJULISHE NA MWENZIO.

ASANTENI SANA NA MUNGU AWABARIKI

"SAIDIA GONGO LA MBOTO"

CHADEMA WAANDAMANA, MJI WA MWANZA WASIMAMA!


Taarifa kutoka jiji la Mwanza zinasema kuwa Chadema wameandamana kama walivyopanga na mji umesimama kwa muda kufanya shughuli nyingine ili kushiriki katika msafara huo, ambao unaelezwa kuwa na waendesha pikipiki wengi na magari.

Monday, February 21, 2011

WAZIRI MKUU ASHIRIKI IBADA YA KUMSIMIKA ASKOFU WA BUNDA RENATUS NKWANDE

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi zawadi ya picha Askofu wa Jimbio la Bunda Renatus Nkwande katika Ibada ya kumsimika Askofu huyo kwenye viwanja vya kanisa katoliki parokia ya Bunda jana.

Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.

MAKAMU WA RAIS APOKEA UJUMBE KUTOKA KWA RAIS MUGABE

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na Naibu Waziri Mkuu wa Zimbabwe Mhe. Thokozani Khupe wakati Naibu waziri huyo alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo, kwa ajili ya kumkabidhi ujumbe maalum wa Rais Kikwete kutoka kwa Rais wa Zimbabwe Mhe. Robert Mugabe unaoelezea juu ya maendeleo na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika miaka miwili ijayo Nchini Humo.

Dk. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na Naibu Waziri Mkuu wa Zimbabwe Mhe. Thokozani Khupe. Alipofika Ofisi kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo, kwa ajili ya kumkabidhi Ujumbe Maalum wa Rais Kikwete, kutoka kwa Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe.

Picha kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KUSIKITISHWA NA TUKIO LA MILIPUKO YA MABOMU LILILOTOKEA GONGO LA MBOTO JIJINI DAR ES SALAAM TAREHE 16 FEBRUARI, 2011

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) inaungana na Watanzania wote nchini kuomboleza maafa yaliyotokea kufuatia milipuko ya mabomu katika ghala la kuhifadhia silaha katika kambi ya Jeshi la wananchi (JWTZ) iliyopo Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.

Tume imesikitishwa na tukio hilo ambalo kutokea kwake kumesababisha uvunjifu wa haki za msingi za binadamu ambazo ni haki ya kuishi na haki ya kumiliki mali.

Ni wazi kuwa milipuko hiyo imegharimu maisha ya watu ambapo mpaka sasa inakadiriwa watu wapatao 23 wameripotiwa kufa na kuacha mamia ya watu wakiwa wamejeruhiwa vibaya, baadhi yao wakibaki bila makazi.

Aidha, Tume inampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na wadau wote yakiwemo mashirika na wananchi kwa hatua za haraka walizozichukua kuwahami waathirika wa milipuko hiyo kwa kuwapatia misaada na huduma zinazostahili.

Wakati huo huo, Tume inatoa wito kwa Kamati ya Ulinzi na Usalama iliyoundwa na Rais kuzingatia misingi ya Utawala Bora wakati wa kutoa huduma na fidia kwa waathirika, kwani kumekuwa na tabia kunapotokea matukio kama haya watu wasio waadilifu hutumia nafasi hii kwa mamlaka waliyopewa kutotenda haki kwa waathirika na badala yake hujinufaisha wao wenyewe na wale wanaostahili kupata haki wanabaki mikono mitupu.

Tunawapa pole wale wote walioathirika na milipuko hii na tunawaomba wawe wavumilivu katika kipindi hiki kigumu wakati serikali ikiandaa taratibu za fidia.

Jaji Kiongozi (Mstaafu) Amiri Ramadhani Manento


MWENYEKITI

21. 02. 2011

KILI YAWEKA HAZALANI MAJINA YA WATAKAO WANIA TUZO

Meneja wa Kinywaji cha Kilimanjaro George Kavishe, akiongea jambo kwa Waandishi wa Habari.
Lloyd 2hungu, kutoka kampuni ya Innovey Auditors (kulia), akimkabidhi kalatasi yenye majina ya waliochaguliwa kuwania tuzo hizo, Mratibu wa Tuzo za Kilimanjaro Musica Awards, kutoka Baraza la Sanaa Tanzania ( BASATA), Angelo Luhala.
Angelo Luhala akisoma majina ya washirki wa tuzo hizo.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakijaribu kuweka kumbukumbu za tukio hilo.

KAMPUNI ya vinywaji ya Tanzania Bruwers Limited (TBL) kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro, ambayo ndiyo inadhamini tuzo za Kilimanjaro Musica Awards 2011.
Mapema leo imetangaza majina ya wasanii watakao wania tuzo hizo. Tukio la kutaja kwa majina hayo lilifanyika Makao makuu ya ofisi hizo Ilala jijini Dar es Salaam, chini ya meneja wa kinywaji hicho George Kavishe na mratibu wa tuzo hizo kutoka Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Angelo Luhala. Akizungumza mbele ya waandishi wa Habari Kavishe alisema kuwa majina hayo yamependekezwa chini ya usimamizi wa kampuni ya Innovex Auditors, huku majina hayo yakikabidhiwa kwa mmoja wa wahusika kutoka kampuni hiyo Lloyd Thungu. Luhala alianza kwa kutaja wasanii watakao shindana kuwania tuzo ya msanii wa kike bora kwa mwaka huu watachuana kati ya Judith Wambura “Lady Jay Dee”, Mwasiti Almasi, Astelina Sanga ‘Linah’, Salah Kaisi ‘Shaa’ na Khadija Omari Kopa ‘Khadija Kopa’. Kwa upande wa msanii Bora wa kiume ni ‘20%’, Ali Kiba, Elius Barnaba, Naseeb Abdull ‘Diamond’, Ambwene Yeseya ‘AY’ na Bell 9. Mwimbaji Bora wa Kiume ni ‘20%’, Barnaba, Ali Kiba’ Banana Zorro, Bell 9 na Diamond. Mwimbaji Bora wa Kike ni Lady Jay Dee, Linah, Mwasiti, Khadija Kopa na Shaa. Wimbo Bora wa Taarab My Valentine wa Jahazi Modern, Top in Town wa Khadija Kopa, Achani Kuniandama Isha Ramadhani Mashauzi Langu Rohini Jahazi Morden na Mama nipe Radhi wa Isha Mashauzi. Wimbo Bora wa Mwaka Mama Ntilie Gelly wa ryames feat AT & Ray C, Sina Raha Sam wa Ukweli, Ya Nini Malumbano 20%, Mkono mmoja Chege & Temba Feat Wahu, Bado Tunapanda Tip Top Conection na Tamaa Mbaya 20%. Wimbo Bora wa Kiswahili (Bandi) Shika ushikapo Mapacha watatu feat Mzee Yusuf, Laptop Extra Bongo, Kauli Twanga Pepeta, Mapenzi hayana Kiapo Twanga Pepeta na Pongezi kwa wanadoa Akudo Impact. Wimbo Bora wa R&B We ni wangu Bell 9, Nikikupata Ben Poul, Hello Hussein Machozi feat Maunda Zorro , Atatamani Linah na Kisiwa cha Malavidavi Z Anton. Wimbo Bora wa Hip Hop Propaganda wa Fid Q, Karibu Tena wa John Makini,Ukisikia Paah wa JCB Feat Fid Q & Chid Benz, Usije Mjini wa AY & Mwana FA na Higher wa Nick wa Pili Feat Joh Makini. Wimbo Bora wa Raggae Sauti ya Rasta wa Ras Rwanda Magere, Misingi ya Rasta ya Worriers From The East, Sayuni ya Jhiko Man, Ujio Mpya ya Hardmad feat Enika & BNV, Reggae Swadakta ya Bob Lau Mwalugaja na What u Feel Inside ya Hardmad. Wimbo Bora wa Ragga/Dancehall Nimefulia wa Benjamin Mambo Jambo feat AT, Action wa CPWAA,Dully,Ngwear na Ms Trnity, Far Away ya Big Jah Man feat Richard, My Friend wa Benjamin na Kiuno weak busy ya Jet Man. Repa Bora wa Mwaka Ferguson, Khalid Chokora, Toto ze Bingwa na Kitokololo. Msanii Bora wa Hip Hop Fid Q, Joh Makini, Ngwear, Chid Benz na Godzilla. Wimbo Bora wa Afrika Mashariki Nitafanya wa Kidumu & Jay Dee, Kare wa P-Unit, Songambele wa Alpha feat AY, Vuvuzela wa Goodlife na Kasepiki wa Bebe Cool. Mtunzi Bora wa Nyimbo 20%, Barnaba, Lady Jaydee, Mrisho Mpoto na Mzee Yusuf. Mtayarishaji (producer) Bora wa Nyimbo wa Mwaka Marco Chali, Lamar, Man Water, Bob Junior na Pancho Latino. Video Bora ya Muziki ya Mwaka Mama Ntilie ya Gelly wa Ryames feat AT & Ray C, Action wa CPWAA, Dully, Ngwear, Ms Trinity, Mbagala wa Diamond na Shoga wa Shaa. Wimbo Bora wa Afro Pop Mama Ntilie wa Gelly wa Ryames feat AT & Ray C, Oyoyo wa Bob Junior, Ya Nini Malumbano wa 20%, Tamaa Mbaya wa 20% na Mbagala wa Diamond. Msanii Mpya anayechipukia Sam wa Ukweli, Linah, Sajna, Bob Junior na Top C. Wimbo Bora wa Kusirikisha/ Kushirikishwa Mama Ntilie wa Gelly wa Raymes feat AT & Ray C, Mkono mmoja wa Chege na Temba feat Wahu, Ahmada wa Offisidetrick feat Bi Kidude,Ukisikia Paah wa JC feat Fid Q & Chid Benz & Jay Moe na Dakika Moja wa FA & AY Feat Hardmad. Wimbo Bora wa Asili Tanzania Adela wa Mrisho Mpoto, Kariakoo wa Maluma, Ahmada wa Offisidetrick feat Bi Kidude,Shangazi wa Mpoki feat Cassim na Wa mbele mbele wa Ommy G. Wimbo Bora wa Zouk/ Rhumba Sina Raha wa Sam wa Ukweli, Ulofa wa Top C, Nabembelezwa wa Barnaba, Bado Robo Saa wa Amini na Bora Nikimbie wa Linah.

Saturday, February 19, 2011

FILAMU YA SHOGA STOP

MWANDAAJI wa Filamu, Hisani Muya, maarufu kama, 'Tino', amesema kuwa amesikitishwa na Wizara kuizuia filamu yake ya Shoga, aliyoikamilisha na kuizindua siku za hivi karibuni.
Akizungumza na Sufianimafoto, kwa njia ya simu, alisema kuwa amepokea taarifa hiyo kwa masikitiko makubwa kutokana na kuwa tayari amekwishatumia gharama kibao katika kuiandaa ikiwa ni pamoja na uzinduzi uliofanyika Februari 4 mwaka huu, jijini Dar es Salaam.
Aidha alisema kuwa alikuwa tayari akifanya maandalizi ya kwenda kuizindua Jijini Mwanza, lakini kutokana na agizo hilo la wizara imembidi asubiri majibu ya Wizara hiyo kuwa aendelee na utaratibu ama la na kuwa anahitaji kuifanyia marekebisho katika sehemu gani.
"Lakini iwapo watasema kuwa haifai basi nitawasikiliza ila tayari nitakuwa nimeshapata hasara ya kuiandaa hadi ilipofika.

AGIZO LA WIZARA
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imeiagiza Kampuni ya kutengeneza filamu ya 'Al-Riyamy Production Company' kuwasilisha Filamu ya 'Shoga' kwa Bodi ya Taifa ya Ukaguzi wa Filamu kwa ajili ya ukaguzi.

Aidha Kampuni hiyo pia imeagizwa kutoisambaza Filamu ya 'Shoga' na kusitisha hatua nyingine yoyote kuhusiana na filamu hiyo hadi hapo Bodi ya Taifa ya Ukaguzi wa Filamu itakapojiridhisha kuwa filamu hiyo inakidhi kuonyeshwa hadharani kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Filamu na Michezo ya Jukwaani Namba 4 ya mwaka 1976.

Kampuni hiyo inatakiwa kuwasilisha kanda hiyo kabla ya februari,17 Mwaka huu, Kwa mujibu wa Sheria hiyo hairuhusiwi kutengeneza filamu bila kupata kibali cha kutengeneza filamu.

Aidha kifungu cha 4 (1) kinaelekezwa bayana kuwa kila anayetengeneza filamu anatakiwa kuwasilisha maombi kwa maandishi kwa Waziri chini ya Sheria hii yakiambatana na mswaada na maelezo ya filamu inayotarajiwa kutengenezwa.
Pamoja na mambo mengine katika kifungu cha 14 (2) Sheria inaipa Bodi ya Filamu mamlaka ya kukagua filamu, picha ya matangazo au maelezo yake kwa makusudi ya kuamua kuonyesha na ikiwarushusu itatolewa maonyesho yawe kwa
namna gani.
Katika Sheria hiyo kifungu cha 15 (1) kinapiga marufuku kwa mtu yoyote kuongoza, kusaidia , kuruhusu au kushiriki katika maonyesho ya filamu bila kuwa na kibali cha Bodi.Sheria hii ilipitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa waraka Namba 22 wa mwaka 1974.

Imetolewa na Kitengo cha Habari, Elimu na MawasilianoWizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo februari,14 mwaka huu.

WAHANGA WA MABOMU WAENDELEA KUFARIJIWA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal, akimfariji Mohamed Rashid Mkaazi wa Majohe mmoja kati ya majeruhi walioathirika na milipuko ya mabomu iliyotokea juzi usiku kwenye Ghala la kutunzia silaha katika kambi ya JWTZ Gongolamboto jijini Dar es salaam, wakati alipotembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili leo, kwa ajili ya kuwafariji majeruhi hao.

Saida Rajab (36) mkazi wa Ukonga Mombasa, akiwa amelazwa kwenye wodi ya Mwaisela Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kukatwa mkono na moja ya bomu lililosababishwa na milipuko ya mabomu yaliyokuwa yamehifadhiwa kwenye ghala la Silaa katika kambi namba 511 KJ ya Jeshi la Wananchi (JWTZ), Gongolamboto juzi.Agnela Mwangoma, ambaye pia ni mmoja kati ya majeruhi waliolazwa hospitali ya Muhimbili, akiwa amewekewa vyuma mkononi.

Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, akimjulia hali mtoto Zuena Issa, mkazi wa Kitunda, aliyelazwa kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Baadhi ya Scout, wakibeba magodolo kupanga katika ukumbi wa PTA baada ya kufikishwa mahala hapo na wasamaliawema waliotoa msaada huo kwa ajili ya watoto ambao bado hawajaonana na wazazi wao, wanaoendelea kushi mahala hapo chini ya Red Cross.

Baadhi ya watoto ambao bado wapo katika ukumbi huo wakisubiri kuja kuchukuliwa na wazazi wao.
Watoto wengine walikuwa wakijifariji kwa kucheza kiduku kama mtoto huyu anavyoonekana akiwaburudisha wenzake.

Hii ni baadhi ya misaada iliyofikishwa katika ukumbi huo leo mchana.

Baadhi ya vijana wanaotoa huduma ya Scout katika ukumbi huo.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, akizungumza na watoto waliokusanywa katika Banda la PTA Sabasaba leo mchana, wakati alipowatembelea watoto hao waliopoteana na wazazi wao kutokana na mlipuko wa mabomu.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sadiq, akizungumza na baadhi ya wazazi waliofika katika ukumbi wa PTA, ambao bado hawajawapata watoto na ndugu zao. Lakini idadi ya wazazi wanaoendelea kuwatafuta watoto wao inaonekana kuwa bado ni kubwa ukulinganisha na idadi ya watoto waliosalia katika ukumbi huo ambao ni jumla ya watoto 18 tu.

Wazazi walifika kutafuta watoto wao wakimkiliza Kamanda wa Polisi, Suleiman Kova.

Baadhi ya watoto hao wakipata msosi, ukumbini humo.

Picha: Sufianimafoto Blog...

UBOVU WA BARABARA DAR- MASASI

Abiria wakijitahidi kusukuma ili kulinasua basi namba T357 BMF lililokuwa limekwama katika eneo la Malendega jirani na Nangulukuru mkoani Lindi. Usafiri wa kusini umezidi kuwa mgumu kutokana na eneo hilo kutokamilika ujenzi wake.

Baadhi ya abiria ambao walikwama katika eneo la Malendega jirani na Nangulukuru mkoani Lindi wakiwa hawana la kufanya..



Kondakta wa basi la Safari Coach (kushoto mwenye shati la bluu) ambalo namba zake hazikupatikana kutokana na kuzibwa na matope, akijitahidi kusawazisha sehemu ili basi hilo liweze kujinasua katika tope eneo la Malendega jirani na Nangulukuru mkoani Lindi.

Thursday, February 17, 2011

INATISHIA AMANI GONGO LA MBOTO

Rais JK akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kufika sehemu ya tukio.
Picha ikionyesha Uwanja wa Ndege wa Taifa.
Baadhi ya wasafiri wakiwa wamejazana uwanjani hapo wakisubiria hadi hari ya hewa ikiwa shwari ili waweze kusafiri.
Waziri wa Ulinzi na Usalama Hussen Mwinyi, akiongea na waandishi wa habari ndani ya kambi ya Jeshi ya Gongo la Mboto mapema leo.
Moja ya jengo la darasa la Shule ya Pugu likiwa limevunjwa na bomu.
Nyumbailiyokumbwa na dhahama ya mabomu.
Baadhi ya maaskali wakiwa wamebeba mabomu, yaliyosalia baadada ya kudondoka Uwanja wa ndege.
Mkuu wa Majeshi nchini (kulia), akiongea jambo na wafuasi wake.

Waandishi wa Habari na wanajeshi wakisikiliza Hotuba ya Rais.
Moja ya nyumba iliyoasiliwa na Mabomu.
Bomu likiwa nje ya nyumba ya mkazi.
Baadhi ya wakazi wa Gongo la Mboto wakisikiliza majina ya watoto wao, kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Raia wakiwa kwenye hari ya huzuni Kiwanjani hapo.
Moja ya Bomu likizagaa.
Moja ya nyumba iliyosambazwa na bomu.
Bomu likiwa mbele ya nyumba ya mtu.
Bomu likiwa limejichimbia chini ya mti karibu na makazi ya watu.
Moja ya baki la Bomu, likizagaa kwenye makazi ya watu.
Bomu likioneka kama limesimikwa na mtu ndani ya nyumba hiyo.
Moja ya Bomu likiwa kwenye uzio wa nyumba.
Baadhi ya raia wa Gongo la Mboto wakitapata barabarani.
Mmoja wa maaskali akiwa amebeba mtoto ambaye mama yake hajapatikana
Huyu naye mama yake hajaonekana.
Baadhi ya watoto walinusulika wakiwa kwenye hema katika Uwanja wa Uhuru.
Mmoja wa Waasilika wa mabomu akiwa amezilai
Msalaba mwekundu wakimpa msaada.
Mmoja wa waasilika wa Mabomu, akisaidiwa na watu wa Msalaba Mwekundu baada ya kuzimia.
Baadhi ya Nyumba iliyoasilika kwa mabomu.
Baki la Bomu likiwa nje ya nyumba ya mkazi mmoja.
Baadhi ya Wahanga wa Mabomu wakiwa Uwanja wa Uhuru.
Rais JK Kikwete akisikiliza chanzo cha mabomu hayo kutoka kwa msemaji wa Kikosi hicho, kambini hapo.
Baadhi ya wakazi wa Gongo la Mboto wakiwa juu ya Daradara tayali kwa kukimbia mabomu.
Mmoja wa waendesha Boda Boda akisafirisha abiria wake.
Wengine wakihama familia nzima kwa kutumia Boda Boda.
Hawa nao wakijikokota kwa miguu kuelekea Uwanja wa Uhuru.
Hari iko hivi Gongo la Mboto kwa leo