Social Icons

Wednesday, January 19, 2011

WAZIRI WA AFYA KUFANYAKAZI NA MABALOZI WA MALARIA NO MORE

Waziri Wa Wizara ya Afya Haji akiwa katika picha ya pamoja na mabalozo 10 wa mradi wa kupambana na Malaria, Zinduka Malaria No More.
Aunt Sadaka Said akizungumza na Waziri mara baada ya kukaribishwa ofisini kwake leo mchana


Baadhi ya Mabalozi wa Mradi wa Zinduka Malaria No More , Lady Jaydee, Barnaba , Profesa Jay wakiwa katoka Ofisi ya Wazuriri wa Afya walipofika kumtembelea leo mchana.


Sadaka Said akimkabidhi Waziri Haji Mponda kabrasha lenye maelezo yanayoeleza jinsi Mabalozi wa Mradi wa Zinduka Malaria No more walivyo fanya kazi kwa kipindi cha mwaka jana.

Na Mwandishi Wetu
Waziri wa Wizara ya Afya Haji Mponda jana ametoa rai kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya ambao pia ni Mabalozi wa Mradi wa kupambana na ugonjwa wa Malaria Zinduka ‘Malaria No More’ kutunga nyimbo zitakazoleta hamasa ya kubadili tabia iliyojengeka miongoni mwa watu ya kuudharau ugonjwa wa Malaria.
Mponda alisema kwamba wasanii hao watafute njia mpya ya kusambaza ujumbe kutokana na tabia iliyojengeza miongoni mwa watu wengi kudharau kujitibu Malaria ugonjwa mbao unaua kwa haraka zaidi hasa wanawake na watoto.
“Utaona mama anaona mtoto ana dalili zote za Malaria lakini atakachofanya ni kumpatia dawa za kutuliza maumivu na kuendelea na shughuli zake kadhalika kwa vujana wenzenu nao wanaoongoza kwa kudharau utakuta mtu akijisikia ana dalili zote za Malaria atapata kinywaji chake na kwenda zake tofauti akiwa anasumbuliwa na magonjwa kana Kaswende hapo atajitibu kwa haraka zaidi” alisema Waziri.
Aidha Waziri aliendelea kwa kutoa shukurani na pongezi za dhati kwa waasisi wa mradi huo.
Wakati huohuo Profesa Jay alizunguymza kwa niaba ya wasanii wengine na kumwomba Waziri kufanya kazi pamoja na kundi hilo la Mabalozi wa Malaria.
“Mheshimiwa Wazuru tunakuomba wewe kwa niaba ya serikali kujiunga na sisi ili tuweze kuongeza nguvu kwa kushirikiana pamoja katika kutokomeza Malaria”.
Naye Waziri alijibu ombi hilo kwa kusema “mimi niko pamoja na ninyi kwa sababu mimi ni mtafiti sayansi na nilisomea mambo hayo hivyo tutakwenda sambamba na kufanya kazi kwa pamoja kadhalika mimi ndiye muasisi wa miradi ya malaria nchini” alisema.
Waziri aliyasema hayo jana wakati akizungumza na Mabalozi kumi wa Mradi huo wa Malaria ambao walikwenda kumtembelea katika Ofisi ya Waziri Dar es Salaam, Mabalozi hao ni Profesa Jay, Lady Jaydee, Fid Q, Barnaba, Marlow, Mwasiti, Diamond, Amini, Banana, B Twelve.
Wasanii hao ambao tayari wameweza kufanya kazi ya kupeleka ujumbe kwa jamii juu ya kujikinga na madhara ya ugonjwa wa Malaria wanatarajia kuanza kusafiri tena mikoani baadaye mwezi ujao.

0 comments: