Mgunga Mwa Mnyenyelwa (aliyesimama kushoto), akitoa ufafanuzi juu ya tamthiliya ya “Nguzo Mama” inayotarajiwa kuonyeshwa tarehe 28 na 29 Januari mwaka huu kwenye ukumbi wa kituo cha utamaduni cha Urusi.
WASANII mbalimbali wakiwemo wacheza filamu, wachoraji, wanamuziki na wachongaji vinyango na sanamu, leo wamepata elimu ya sanaa ya maonyesho na kuhamasishwa kupima afya zao na jinsi ya kuepuka kukumbwa na ugonjwa wa ukimwi.
Akizungumza katika hafla ya Jukwaa la Sanaa lililofanyika katika ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Mkurugenzi Mtendaji wa Parapanda Theatre Lab Trust, Mgunga Mwa Mnyenyelwa, amewataka wasanii wote kuwa na dira katika kazi zao kabla ya kutoa kazi akawataka wafanye utafiti ili kujua kile wanachokifanya kama kitanufaisha taifa
Aidha aliendelea kusema kuwa kikundi hicho kina malengo ya kuwasaidia wasanii wa Bongo Fleva ili waweze kuimba nyimbo zao zikiwa na mguso wenye asili ya Kiafrika kwa lengo la kuzitofautisha na za nchi nyingine.
Naye, mshauri kutoka shirika la AMREF, Bahati Mwitula, aliwapa somo wasanii hao na kuwahamasisha kupima afya zao ambapo alisema kuwa shirika hilo limeamua kuwafuata watu pale walipo na siyo mpaka watu wawafuate wao.
Wasanii wakisikiliza kwa makini mafunzo.
Bahati Mwitula (aliyesimama) akijitambulisha kwa wasanii.
……Akifafanua jambo kuhusu ukimwi.
0 comments:
Post a Comment