Michael Wage akiondoka mahakamani baada ya kukiri kutoa rushwa ya shilingi milioni 10.
Na Richard Bukos
ALIYEKUWA Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Michael Wage, ambaye kwa sasa ni mlalamikaji na shahidi wa kwanza katika kesi ya kutaka kupokea rushwa ya shilingi milioni 10 inayomkabili mtangazaji wa kituo cha luninga cha Taifa (TBC1), Jerry Muro, amekiri kutoa rushwa ya kiasi hicho cha pesa.
Wage alisema hayo baada ya kubanwa na wakili wa upande wa utetezi, Majura Magafu, aliyemtaka kuelezea lengo la kutoa shilingi milioni moja alizodai kuwapa Jerry Muro na wenzake.
Mlalamikaji huyo alisema aliwapa Jerry Muro na wenzake kiasi hicho fedha ili wasirushe hewani kwenye kipindi cha ‘Usiku wa Habari’ tuhuma za matumizi mabaya fedha kwenye Halmashauri ya Bagamoyo.
Magafu alimueleza Wage kuwa kitendo chake cha kueleza mahakamani kuwa alitoa rushwa ili tuhuma zake zisirushwe kwenye luninga kinathibitisha kuwa mlalamikaji huyo ana kesi ya kutoa rushwa, hivyo kosa hilo linaweza kumpeleka jela.
Kesi hiyo iliyounguruma leo inatarajiwa kuendelea tena mahakamani hapo kesho, Jumanne, mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Gabriel Mirumbe.
Jerry Muro, akiondoka mahakamani.
0 comments:
Post a Comment