Social Icons

Saturday, January 15, 2011

ATLETICO PARANANSE YA BRAZIR YATUA DAR


Katika picha katikati ni makam wa Rais wa timu hiyo Roberto Karam.

Rais wa Klabu ya African Lyon ya jijini Dar es Salaam, Nabil Salim, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano uliofanyika kwenye Hoteli ya Moven Pick, kuhusu ujio wa timu ya Atletico Parananse kutoka nchini Brazir. Timu hiyo inadaiwa kuwa ni miungoni mwa timu zinazoishiriki Ligi Kuu ya nchini humo, imekuja kucheza michezo ya kirafiki na timu za Yanga na Simba.
Mchezo wa kwanza utakuwa ni kati ya timu ya Yanga utakaochezwa Januari 18 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifajinini Dar, na mchezo wa pili itakuwa kati ya timu hiyo na Simba mchezo utakaochezwa Januari 20 katika uwanja huohuo.


Makamu wa kwanza wa Rais wa TFF, Athuman Nyamlani, (katikati), akielekezana jambo na mkuu wa Idara ya Soka la kulipwa wa timu hiyo, Luiz Fernando Cordeiro na Ahmed Ali Al-Shirazi wa timu ya African Lyon.

Baadhi ya wachezaji wa timu hiyo wakiingia kwenye Hoteli ya Moven Pick, baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam jana usiku.

Rais wa Klabu wa African Lyon, Nabil Salim (kulia) akisalimiana na baadhi ya viongozi kutoka ubalozi wa Brazil.

Baadhi ya wachezaji wa timu hiyo wakiwa wamepozi hotelini hapo jana usiku.

Picha: Sufianimafoto Blog.

0 comments: