Social Icons

Monday, October 11, 2010

MOROCCO ILIVYO JIPATIA BAO ZIDI YA TAIFA STARS!!

Mshambuliaji wa Morocco, Chamakh Marouane anayeichezea klabu ya Arsenal ya Uingereza akipangua ngome ya Stars katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Pilika pilika za kuwania mpira.
Timu ya Taifa ya Morocco imeweza kujipatia pointi muhimu na goli la ugenini baada ya kuifunga Taifa Stars bao 1-0 katika mchezo wao uliopita katika Uwanja wa Taifa jijini Dar. Alikuwa mshambuliaji Mounir El-Hamdaou wa Morocco aliyefunga bao hilo pekee la mchezo kwa shuti kali toka mguu wa kushoto, lililomshinda mlinda mlango Juma Kaseja, dakika mbili tu kabla ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza. Hii ilikuwa ni mwendelezo wa ratiba ya mechi za kufuzu kucheza fainali ya kombe la Mataifa ya Afrika ambapo katika mechi iliyotangulia iliyochezwa nchini Algeria hapo Septemba 3, 2010, Tanzania walipata pointi muhimu ya ugenini japo walitoka sare ya bao 1 - 1 dhidi ya wenyeji wao.Tanzania imepangwa kundi moja la D, na timu za Algeria, Morocco na Jamhuri ya Afrika ya Kati. Mgeni rasmi katika mechi hiyo alikuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mdau mkubwa wa michezo, Jakaya Mrisho Kikwete ambaye alisitisha kampeni za uchaguzi mkuu ili kuhudhuria mechi hiyo.

0 comments: