Miss Progressive Julieth William.
Richard BukosKampuni ya SYSCORP Media iliyoratibu Mashindano ya Miss Progressive hapa Bongo yaliyofanyika nchini Itali mwishoni mwa mwezi uliopita na mrembo Julieth William kuibuka na taji la dunia, Jumatano iliyopita ilitembelewa na wasimamizi wa kimataifa wa makampuni ya wajasiriamali barani Afrika.
Hatua hiyo ilikuja kufuatia kampuni hiyo kufanikiwa kuingia kwenye 15 bora baada ya kushindanishwa kwa makampuni 2700 Barani Afrika.
Afisa Mtendaji Mkuu wa SYSCORP Media, Beatus Kaboja aliupokea ugeni huo kutoka nchi za Marekani na Australia na kuwapa siri mbalimbali za mafanikio ya kampuni yake.
Baada ya kuwapa siri ya mafanikio ya kampuni hiyo, Kaboja aliwatembeza wasimamizi hao katika maeneo tofauti ya uzalishaji pamoja na kukagua mapato ya kampuni hiyo.
Hata hivyo, taazifa zilizopatikana baadaye zilieleza kuwa baada ya SYSCORP Media kuingia 15 bora fainali za kupata tatu bora na mshindi wa kwanza zitafanyika Nairobi nchini Kenya, Desemba 6, mwaka huu ambapo mshindi wa kwanza ataibuka na kitita cha dola za kimarekani laki moja.
0 comments:
Post a Comment