Social Icons

Wednesday, September 29, 2010

TANZANIA MODELS KUFANYA ONYESHO LA MAVAZI ARUSHA!!!


KIKUNDI cha Wanamitindo kijulikanacho kwa jina la 'Tanzania Models Group' wanatarajia kufanya onyesho la mavazi katika ukumbi wa Via Via Club jijini Arusha litakalofanyika jumamosi. Akizungumza na Dimba Mratibu wa onyesho hilo lililopewa jina la 'Time and Beauty' Bi. Angel Justace alisema kuwa lengo la kuandaa onyesho hilo ni kuweza kutangaza umoja wao, kuvumbua vipaji vya vijana na kutangaza Utalii wa nchi ya Tanzania. Bi. Angel Justace alisema kuwa kwa sasa wakati umefika kwa vijana kuungana katika kutangaza utalii wa nchi. "Sisi kama vijana hatuna budi kujitoa kwa kuungana na kutangazaa Utalii wa nchi yetu, kwani bila kufanya hivyo nchi yetu haiwezi kutambulika na wageni hawawezi kujua nchi yetu ina vivutio gani vinavyovutia," Onyesho hilo linalotarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Via Via Club litawakutanisha wanamitindo kutoka Dar es Salaam na jiji la Arusha huku wakipabwa na mbunifu wa mavazi ya asili Bw. Gabriel Mollel Sairiamu. Aliongeza kuwa mbali na mbunifu huyo wa mavazi ya asili Bw. Gabriel Mollel Sairiamu pia atakuwepo msanii wa kizazi kipya Hussein Machozi. Onyesho hilo limedhaminiwa na Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro Conservation-Arusha, Kilimanjaro Express Bus, Mwandago Evestiment, Coco Pazzo, Triple A Radio na Masai Club ya Dar es Salaam.

0 comments: