Social Icons

Monday, September 6, 2010

FM ACADEMIA KUZINDUA ALBAM YA PILI IDD MOSI !!

Mmoja wa wanenguaji wa FM Academia akiwajibika jukwaani.

Lily akitetea msosi wake baanaa!!!!!!!!
Setephanie akitikisa mkia.

BENDI ya Muziki wa Dansi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ imekamilisha matayarisho yote kuelekea uzinduzi wa albamu yao mpya iliyopewa jina la Vuta Nikuvute Mathematics, inayotarajiwa kuzinduliwa wakati wa Sikukuu ya Idd El Fitr wiki hii. Rais wa bendi hiyo, Nyoshi El Saadat ameiambia Mateja20 Entertainment Mix kuwa event nzima itakuwa ndani ya Ukumbi wa Diamond Jubilee, siku ya Idd Mosi na kwamba wamejipanga vilivyo kuwaburudisha mashabiki wake, baada ya kumaliza mfungo wa mwezi mtukufu.
“Tunafanya mazoezi usiku na mchana kuhakikisha siku hiyo tunazikonga vilivyo nyoyo za mashabiki wetu, hakika nawaambia waje kwa wingi Diamond Jubilee wajionee shughuli pevu ya wazee wa Ngwasuma tukiwa na Nameless kutoka Kenya,” alisema Nyoshi.



0 comments: