Social Icons

Monday, August 9, 2010

RAHA ZA FIESTA 2010

Kila aliyehudhuria onesho la Fiesta 2010 (Jipanguse - Rraaa ) aliondoka na tabasamu kwa kukubali kwamba kilichofanyika juzi (Jumamosi) kwenye Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, Dar haijawahi kutokea kwani ilitisha kwa matukio na burudani.

Lil Kim na Sir Nature wakifanya mambo jukwaani
Alichokifanya mwana Hip Hop wa Marekani aliyekatikiwa mshipa wa aibu, Kimberly Denise Jones ‘Lil Kim’ jukwaani na Mfalme wa Temeke, Juma Kassim Kiroboto ‘Sir Nature’, tukio la staa wa Clouds FM, Fatma Hassan ‘DJ Fetty’ kupigana na mengineyo ni vichache kati ya vionjo vingi vya Fiesta 2010.

Dj Fetty akizipiga na mdada
The Biggest IQ Paper, Ijumaa Wikienda lina mzigo kamili, kwani lilikuwepo Leaders kuchukua sinema kamili iliyoanza Jumamosi majira saa 9 alasiri na kipimo cha kwanza kinachosherehesha kuwa Fiesta 2010 ilikuwa ‘next level’ ni umati wa kihistoria uliohudhuria shoo hiyo.

...Wengine walipoteza 'memory' kama hivi
Tathmini ya gazeti hili inatoa jibu kuwa Fiesta 2010 imevunja rekodi ya maonesho yote yaliyowahi kufanyika nchini kwa kuanzia idadi ya wahudhuriaji, aina ya jukwaa na kile ambacho kilifanywa na wasanii, hivyo kumfanya kila aliyelipia kiingilio, aondoke akiwa ametii kiu yake.

..Fegi kwa sanaa, pichani ni Malkia Ngwasuma akipuliza moshi
Gazeti hili lenye uzoefu wa kutosha katika kufanya ‘kavareji’ ya matukio ya burudani nchini, linatoa jawabu kuwa jukwaa lililotumika Fiesta 2010 ni kiwango ambacho hakijawahi kutokea Bongo.
Mbali na ukubwa, ‘matirio’ ya jukwaa hilo kuanzia uimara wake, taa na vinginevyo, ni sifa ambazo zinalitofautisha na mengine yaliyotumika nchini.

...'Hands up' kama inavyoonekana pichani
Kituko kilichotia fora ni mwanadada DJ Fetty kutwangana na ‘mdada’ mwingine ambaye anadaiwa ni mfanyakazi mwenzake.
Hata hivyo, chanzo cha warembo hao kutwangana wakati shoo ya Fiesta 2010 ilipokuwa imepamba moto hakijajulikana, lakini ‘mtiti’ wao ulikuwa si wa kitoto.

Lil Kim aliyeanza kutisha tangu miaka ya 90 akiwa na ‘lebo’ ya Bad Boy Entertainment na kuvuma kwa uhusiano wake wa kimapenzi na mwana Hip Hop, marehemu Christopher Wallace ‘Notorious BIG’, alionesha kuelewa hadhira ya Bongo inataka nini na akaipa.

...Mwanadada akidhibitiwa na baunsa
Mwanamuziki huyo mwenye sifa ya ‘uchakaramu’, alipanda jukwaani na kupagawisha kwa kiwango kikubwa lakini alipoona mashabiki wanapunguza shangwe, alimuita Juma Nature ambaye aliungana naye jukwaani.
Kupanda kwa Nature jukwaani na kupiga shoo ya pamoja na Lil Kim, ilikuwa ni mseto wa ambao haujawahi kutokea, hivyo kusababisha shangwe za kiwango cha juu.

Uhodari wa Lil Kim katika kucheza staili ya ‘Mapanga Shaa’, wepesi wa kunengua wimbo wa Nature wa ‘Mugambo’ na kadhalika, ni vitu ambavyo vilimuongezea mwanamuziki huyo alama za kushingiliwa.
Kim, alizidi ‘kuiroga’ hadhira pale alipokuwa anamkumbatia Nature mara kwa mara na kumpiga mabusu, ‘manjonjo’ ambayo yaliamsha kelele.

...hapo vipi?
Kutokana na tukio hilo, muda wote Kim akiwa jukwaani na baada ya kuteremka, mashabiki walikuwa wakipaza sauti, wakimuita mwanamuziki huyo shemeji kutokana na ‘ndoa’ aliyofunga jukwaani na Mfalme wa Temeke.

Kionjo kingine ni kivazi cha Kim ambacho muda wote kilianika kufuli lake, hivyo kuwafanya baadhi ya wenye uchu, kupiga chabo chini ya jukwaa.

Kituko kingine ni mdau wa soka, Nagari Kombo aliyefanya kituko Mei mwaka huu kwa kuingia Uwanja wa Taifa na kumkumbatia staa wa Real Madrid, Mbrazil Ricardo Kaka wakati Timu ya Soka ya Taifa la Tanzania ‘Taifa Stars’ ilipocheza na Brazil, kushtukiwa kwenye jaribio la kumvaa Kim.

Nagari Kombo (Staa wa Kaka) akidhibitiwa na baunsa
Nagari (Staa wa Kaka), alishtukiwa na baunsa anayeitwa Michael Mwanzamwanza wakati akiwa amekwishavuka uzio wa kwanza na kujichanganya na mapaparazi kama geresha, akitafuta njia ya kumfikia mkali huyo wa Hip Hop mwenye jinsi ya kike.
Stadi wa Hip Hop Bongo, John Simon ‘Johmakini’ alidhihirisha umwamba wake wa Kaskazini na kuonesha kuwa ‘swaga’ anazijua kwa kupiga shoo ya kiwango bora.

Wasanii wengine wa Bongo waliotisha jukwaani ni Fareed Kubanda ‘Fid Q’, Wanaume Family, Witness Kaijage, Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’, Sara Kaisi ‘Shaa’, Nassib Abdul ‘Diamond’, Kikosi cha Mizinga, Barnaba na Linah (THT).

Lil Kim akifanya vitu vyake jukwaani
Washereheshaji wa shoo, Adam Mchomvu, Hamis Mandi ‘B12’ na DJ Fetty walitoa burudani ya aina yake ambayo ilipokelewa na shangwe.
Staa wa Misifaz Camp, Abdul Sykes ‘Dully’ hakufanya vizuri jukwaani kutokana na kile ambacho kilibeba tafsiri kwamba amekuwa bonge na uzito kuongezeka.

Wakali kutoka Ivory Coast, DJ Rahmatullah na mwimbaji wa staili ya Aladji, walitegemewa wangefunika lakini ilikuwa kinyume, kwani walifunikwa na wanamuziki hata wa nyumbani.
Kundi la Brackets la Nigeria, nalo lilifanya vizuri kwa kugonga ‘mchanyato’ wa nyimbo zao za zile za Kundi la P-Square.
Kwa jumla, shoo nzima ilipangiliwa vizuri kuanzia mwanzo majira ya saa 9 alasiri (Jumamosi) hadi saa 11 alfajiri (Jumapili).

...ilikuwa ni 'Tanzania make some noise'
Rangi ilipendeza muda wote, ulinzi wa uhakika ulikuwepo ingawa mishale ya saa 8 usiku, wakati mafataki yalipopigwa kumkaribisha Kim, baadhi ya watu ambao hawajazoea hayo mambo (mashikolomageni) walikimbia huku na huko wakidhani ni hatari.
Timu ya Ijumaa Wikienda iliyofanya ‘kavareji’ Fiesta ni Sifael Paul, Richard Bukos, Musa Mateja, Aziz Hashim, Hemed Kisanda na Shakoor Jongo.

0 comments: