Wiki hii tunaye mwanadada aliyejiajiri kwenye kiwanda cha muziki Bongo baada ya kuibukia katika Shindano la Bongo Star Search (BSS). Wengi wanamfahamu kwa jina la Baby Madaha lakini jina lake kamili ni Baby Joseph Madaha.
Alizaliwa Novemba 19, 1986 nchini Msumbiji na kuanza Shule ya Msingi ya St. Gervas iliyopo nchini Kenya hadi Darasa la Nne kabla ya kuhamia Tanzania katika Shule ya Msingi Bugando, Mwanza alikomaliza Darasa la Saba. Baadaye alijiunga na Shule ya Ganza Girls mwaka 2000 hadi alipohitimu Kidato cha Nne mwaka 2004.
Kidato cha Tano na Sita alisoma katika Shule ya Sekondari Kizu kabla ya kujiunga na Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ) kuchukua stashahada ya uandishi wa habari.
Hiyo ndiyo historia yake kwa ufupi, zaidi kuhusiana na mwanadada huyu, ungana nami katika maswali kumi ambayo nilimgonga nayo kisha naye akaonesha ushirikiano wa hali ya juu.
TQ: Kujulikana kwako kulianzia kwenye shindano la BSS, ni kipi kilichokusuma kuingia katika shindano hilo?
BABY MADAHA: Nilikuwa napenda sana muziki na lilipotokea shindano hilo nikaona ni nafasi pekee ya kuonesha kipaji changu, nikashiriki bila kushinikizwa na mtu.
TQ: Mbona sasa hukufanikiwa kuibuka mshindi? Au ulikuwa miongoni mwa wasindikizaji?
BABY MADAHA: Mpaka leo nashindwa kujua kilichonikosesha ushindi lakini wapo majaji waliokuwa wakinikubali kama Madam Ritha.
TQ: Baada ya kupigwa chini katika mchakato huo ulitokomea wapi maana ulikaa kimya muda mrefu.
BABY MADAHA: Wakati nashiriki shindano hilo nilikuwa bado nasoma ‘so’ nilipotolewa nilirudi shule kuendelea na masomo yangu.
TQ: Kulikuwepo na habari kwamba, umechukuliwa na wadosi na kufanya muziki nchini India, ilikuwaje?
BABY MADAHA: Baada ya kumaliza chuo, nilikwenda India kwa lengo la kutengeneza tangazo la pombe, nikiwa kule ndiyo nikakutana na wadosi ambao waliipenda sana sauti yangu na kunipeleka studio.
TQ:Ni mafanikio gani uliyoyapata hadi sasa kupitia muziki?
BABY MADAHA: Nimefanikiwa kuzijua sehemu mbalimbali duniani kupitia muziki, pia kwasasa naishi kwa kujitegemea. Lakini pia nimefanikiwa kujitangaza kupitia muziki hasa ukichukulia kwamba, nimeshakamilisha albamu moja iitwayo Amore na naandaa ya pili inayokwenda kwa jina la Desperado.
TQ: Tugeukie maisha yako ya kimapenzi,umeolewa au una mchumba?
BABY MADAHA: Sijaolewa na kwakweli sina mpango wa kuolewa hivi karibuni.
TQ: Ni mwanaume wa aina gani ambaye ungependa awe mume wako wa maisha wakati ukifika?
BABY MADAHA: Napenda mwanaume mchangamfu, asiwe na wivu wa kijinga na hobi zetu ziendane. Pia awe na uwezo na kamwe siwezi kutoa penzi langu kwa mariyo (mwanaume tegemezi).
TQ: Tumenyetishiwa kuwa unajiachia na mmoja wa mabosi wako, hilo unalizungumziaje?
BABY MADAHA: Duuh! Kuna hilo tena? Anyway isiwe tabu maana watanzania hawakosi la kusema, nilipokuwa BSS walisema napendelewa. Ukweli ni kwamba, sina uhusiano na bosi wangu yeyote zaidi ya kazi tu.
TQ:Kuna tetesi kuwa umezaa mtoto na hutaki watu wajue?Kuna ukweli katika hilo?Je, katika maisha yako ungependa kuzaa watoto wangapi?
BABY MADAHA:Katika maisha yangu nitafurahi sana kama nitapata watoto wawili tena wa jinsi tofauti na kuhusu hilo kuwa na mtoto, siyo kweli!
TQ: Wasanii wengi wanapenda kutumia pombe ama bangi ili kutafuta mzuka wa kupandia jukwaani, wewe huwa unatumia nini?
BABY MADAHA: Kweli nakunywa pombe lakini sipendagi kunywa pombe kabla ya kupanda jukwaani. Ila kama niko sehemu halafu kuna pombe aina ..…(anaitaja) naweza kupata moja tu kabla ya shoo.

0 comments:
Post a Comment