JOSEPHINE URIO
Na Musa Mateja
Shindano la kumsaka mlimbwende wa Mwanza 2010 linatarajiwa kufanyika Juni 18 ambapo Mamiss zaidi ya 16 watatifuana vilivyo kuhakikisha anapatikana mrithi wa Miriam Gerard ambaye anashikilia taji hilo kwa sasa.
Akiongea na safu hii Mkurugenzi wa kampuni ya Sisi Entertainments,John Dotto alisema kwamba shindano hilo litafanyika ndani ya Ukumbi wa Yatch Club jijini Mwanza na litasindikizwa na Belle9,Bob Haisa,Jita Man na wengine kibao ambao atawaja hivi karibuni.
Alisema mashindano hayo yatakuwa chini ya Udhamini wa Vodacom,TBLl(Reds),Global
Publishers wachapishaji wa magazeti ya Ijumaa Ijumaa Wikienda Risasi Championi Uwazi na Amani kupitia bahati nasibu yake ya jishindie gari aina ya Toyota Vitz awamu ya pili 2010.
0 comments:
Post a Comment