Social Icons

Monday, June 7, 2010

JAM SESSION YAZINDULIWA SUN CIRRO


ULE mpango mzima unaohusisha wanafunzi kutoka shule mbalimbali za jijini Dar es Salaam ambao unajulikana kama ‘Jam Session’ ambapo wanafunzi watakuwa wakikutanika na kucheza miziki na sarakasi, jana ulizinduliwa rasmi ndani ya ukumbi wa klabu ya Sun Cirro uliopo maeneo ya Legho, Sinza, jijini Dar es Salaam, kwa onyesho lililofanywa na msanii kutoka nchini Uganda, Michael Ross.

Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na wasanii mbalimbali nchini wanamuziki Witness, AY na wasanii wa filamu, Dokii na Jacky wa Chuzi ambapo Jack Pemba alikiwa miongoni mwa wageni wa heshima. Hafla hiyo ilishereheshwa na mtangazaji mahiri kutoka redio ya Clouds FM, Hamisi Mandi ‘B12’.



Michael Ross akifanya makamuzi ya nguvu katika uzinduzi huo.


Witness naye hakuwa nyuma kuonyesha vitu vyake muda mfupi baada ya kupanda jukwaani.




Mtangazaji wa kipindi cha XXL cha Clouds FM ‘B12’ akiongea jambo katika shughuli hizo.


Witness akiwa na Ombeni wa G5click

0 comments: