Picha: Bongo Star Link...
Wednesday, October 27, 2010
MATONYA AKIFANYA MAKAMUZI NA NONINI
Picha: Bongo Star Link...
SUPA PESA YAZIDI KUMWAGA MAHELA
LILE shindano la Supa Pesa limezidi kuwanufaisha Watanzania baada ya leo kumwaga mahela kwa Bw. Raymond Sinda ambaye alishinda na kujinyakulia kitita cha shilingi milioni kumi. Mshindi huyo alikabidhiwa mfano wa hudi yenye thamani ya pesa hizo na Meneja Mkuu wa Supa Pesa, Natasha Issa, katika ofisi za Odssey zilizopo Masaki Mwisho, jijini Dar es Salaam. PICHANI Raymond Sinda (kushoto) akikabidhiwa mfano wa hundi hiyo.
…….Akiongea na waandishi wa habari.
Baadhi ya waandishi wa habari wakipiga picha wakati wa hafla hiyo.
CCM YADAI KIKWETE KAKASHIFIWA NA CHADEMA
- MENEJA Kampeni wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrhaman Kinana, leo ametangaza nia ya chama chake kukishitaki Tume ya Uchaguzi, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kufuatia mgombea wake wa ubunge, Jimbo la Temeke, Jijini Dar es Salaam, Amos Ng’ili, kumtolea lugha za kejeli na udhalilishaji mgombea urais kupitia chama chake, Dk. Jakaya Kikwete. Kinana amedai leo mbele ya wanahabari kuwa Ngili alimdhalilisha Kikwete kwenye mkutano wa kampeni wa chama chake uliofanyika jana jioni katika viwanja vya Tandika Mwembe- Yanga, jimboni humo ambapo baada ya tukio hilo mgombea urais wa chama chake, Dk. Willbroad Slaa, alimkumbatia na kumpa mkono wa pongezi. Kinana (pichani) alisema hayo wakati akizungumza na wanahabari kwenye ofisi ndogo za CCM zilizopo Barabara Lumumba jijini.
'BABU AJITOSA CCM'
Msanii wa Bongo Flava, Haruna Kahena, a.k.a Inspector Haroun 'Babu' naye ameungana na wasanii wenzake kuipigia debe CCM. Babu, alikuwa miongoni mwa wasanii wa bongo flava waliotumbuiza wakati wa mkutano wa DK. Jakaya Kikwete leo Kiwalani jijini Dar es salaam. Pichani ‘Inspekta Haruni’, akifanya makamuzi katika mkutano huo.
Dk. Jakaya Kikwete (katikati) akielekeza jambo muda mfupi baada ya kuwasili katika mkutano huo. Wa kwanza (kushoto) ni mgombea ubunge wa jimbo hilo, Makongoro Mahanga, wengine ni baadhi ya viongozi wa ngazi mbalimbali wa chama hicho.
Nasib Abdul ‘Diamond’ (mwenye maiki) naye hakuwa nyuma kutumbuiza katika mkutano huo na rafiki yake mapema leo.
Tuesday, October 26, 2010
IGP MWEMA ATOA WITO KWA WANANCHI
Aidha Mkuu huyo , amesema kuwa amani na usalama na utulivu hapa nchini vitadumishwa wakati wote kabla na baada ya uchaguzi, kwa kuhakikisha kwamba sheria , kanuni na taratibu za nchi zinafuatwa ipasavyo.“Tukumbuke kwamba vitendo vyovyote vya uvunjwaji wa sheria, kabla na baada ya uchaguzi ni uhalifu.Sheria haina udhuru, inachukua mkondo wake mara moja endapo ukiukwaji umefanyika. Hivyo kutii sheria na taratibu za uchaguzi ni wajibu wa kila mpiga kura na kila mwananchi,” alisema Mwema.Aliongeza kuwa baada ya kura kupigwa na zoezi hilo kufungwa rasmi, hatua inayofuata ni kuzichambua na kuzihesabu ili kupata matokeo, hivyo huo ndo wakati wananchi wanatakiwa kuwa na subira, kwa sababu zoezi hilo ni muhimu na linapaswa kuendeshwa kwa umakini wa hali ya juu ili, haki itendeke na kuepusha malalamiko.Mkuu huyo alisema baada ya matokeo kutangazwa ni muhimu kutambua kwamba aliyeshinda ndiye aliyepigiwa kura nyingi na watu wengi.“Wote tunawajibu wa kumkubali , kumtambua na kushirikiana naye ili kumsaidia kutimiza wajibu wake kama kiongozi wa watu wote,” alisema.Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarouk Abdulwakil aliwataka wananchi wote bila kujali itikadi au udini kuendelea kuwa na msukumo wa utaifa na kuacha maslahi binafsi ili amani, usalama na utulivu vidumu kabla ya baada ya uchaguzi.Alisema wizara yake inawahakikishia wananchi kwamba nchi itakuwa katika hali ya amani, usalama na utulivu wakati wote huku, hivyo alisisitiza ushirikiano kutoka kwa wananchi .
JOKETI ADAIWA KUMFUATA HASHEEM MAREKANI
Habari kwa hisani ya Bongo Star Link blog...
PWEZA PAUL AFARIKI DUNIA
PWEZA aliyejizolea umaarufu mkubwa kutokana na utabiri wa baadhi ya matokeo ya mechi zilizokuwa zikifanyika siku chache katika michuano ya kombe la dunia, iliyofanyika nchini Afrika Kusini, maarufu kwa jina la Paul, hatimaye amefariki dunia usiku wa kuamkia leo huko nchini Ujerumani alipokuwa akifugwa.




