Social Icons

Wednesday, October 27, 2010

'BABU AJITOSA CCM'

Msanii wa Bongo Flava, Haruna Kahena, a.k.a Inspector Haroun 'Babu' naye ameungana na wasanii wenzake kuipigia debe CCM. Babu, alikuwa miongoni mwa wasanii wa bongo flava waliotumbuiza wakati wa mkutano wa DK. Jakaya Kikwete leo Kiwalani jijini Dar es salaam. Pichani ‘Inspekta Haruni’, akifanya makamuzi katika mkutano huo.

Dk. Jakaya Kikwete (katikati) akielekeza jambo muda mfupi baada ya kuwasili katika mkutano huo. Wa kwanza (kushoto) ni mgombea ubunge wa jimbo hilo, Makongoro Mahanga, wengine ni baadhi ya viongozi wa ngazi mbalimbali wa chama hicho.

Nasib Abdul ‘Diamond’ (mwenye maiki) naye hakuwa nyuma kutumbuiza katika mkutano huo na rafiki yake mapema leo.

0 comments: