- MENEJA Kampeni wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrhaman Kinana, leo ametangaza nia ya chama chake kukishitaki Tume ya Uchaguzi, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kufuatia mgombea wake wa ubunge, Jimbo la Temeke, Jijini Dar es Salaam, Amos Ng’ili, kumtolea lugha za kejeli na udhalilishaji mgombea urais kupitia chama chake, Dk. Jakaya Kikwete. Kinana amedai leo mbele ya wanahabari kuwa Ngili alimdhalilisha Kikwete kwenye mkutano wa kampeni wa chama chake uliofanyika jana jioni katika viwanja vya Tandika Mwembe- Yanga, jimboni humo ambapo baada ya tukio hilo mgombea urais wa chama chake, Dk. Willbroad Slaa, alimkumbatia na kumpa mkono wa pongezi. Kinana (pichani) alisema hayo wakati akizungumza na wanahabari kwenye ofisi ndogo za CCM zilizopo Barabara Lumumba jijini.
Sehemu ya wanahabari wakimsiliza Kinana.
0 comments:
Post a Comment