WIKI YA NENDA KWA USALA ILIYODHAMINIWA NA AIRTEL & ENGINE TZ, YAFANA BUKOBA
Maandamando ya pikipiki yaliyofanyika katika siku ya ufunguzi wa wiki ya Nenda kwa usalama barabara, iliyofanyika mwaka huu kitafia katika Mkoa wa Kagera jumatatu hii 3/10/2011 na kudhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel na kampuni inayouuza mafuta ya Engine Tanzania.
Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mh: Hashim Kagesheki, akimshukuru Meneja wa Kanda ya Ziwa wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel Ally Maswanya, kwa kuwa mdhamini mkuu wa kampeni ya Usalama Barabara kwa mwaka huu, haya yalifanyika katika halfa ya ufunguzi wa wiki ya usalama barabarani katika Mkoa wa Kagera wiki hii na kuhudhuriwa na mgeni Rasmi Mh: Jaji Mkuu Mohamed Chande (katikati) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali mstaafu Fabiani masawe (wakwanza kushoto). wadhani wakuu wa mwaka huu ni kampuni ya simu za mkononi ya Airtel na kampuni ya mafuta Engine Tanzania.
Mbele ni Meneja wa kanda ya ziwa wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Ally Maswanya akipokea cheti maalum kwa airtel ushiriki na shukrani toka kwa kamati na jeshi la usalama barabarani kwa Airtel kuwa mdhamini mkuu wa kampeni ya usalama barabara kutoka kwa mgeni Rasmi Mh Jaji mkuu Mohamed Chande katika halfa ya ufunguzi wa wiki ya usalama barabarani iliyofanyika kitafia katika mkoa wa Kagera wiki hii, wakwanza kulia pichani ni Mwenyekiti wa Baraza la usalama barabarani na Naibu Waziri wa mambo ya ndani Mh Hashim Kagesheki
Bendi ya Kakao ya mkoani Kagera, ikitumbuiza katika siku ya ufunguzi wa wiki ya Usalama Barabara iliyofanyika kitaifa katika Mkoa wa Kagera jumatatu na kudhaminiwa mwaka huu na Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel na Engine Tanzania.
Wednesday, October 5, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment