FAINALI BONGO
STAR SEARCH, KUMDONDOSHA MR FLAVOUR
Mr Flavour akiwa kwenye pozi na mrembo katika moja ya video ya nyimbo zake.
FAINALI ya shindano la kumsaka mkali wa kuimba la Bongo Star Search ‘Second Chance’ 2011, inatarajiwa kuchukua nafasi Oktoba 14, mwaka huu (Ijumaa), ndani ya Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na mtandao huu mapema leo, mkurugenzi wa BSS, Rita Paulsen ‘Madam’ alisema kuwa fainali hiyo itatumbuizwa na msanii mkubwa kutoka nchini
Tiketi zitapatikana kuanzia tarehe 11 katika maduka ya Shee Illussion Mlimani City na Millenium Towers Kijitonyama, Biggy Respect Kariakoo, Steers City Centre, katika maduka yote ya Zizzou Fashion, Beauty Point Shoppers Plaza, Mbalamwezi Beach Club Mikocheni kwa Walioba, Manywele Cosmetics Kinondoni, Best Bite, Engine Mbezi Beach na katika Ukumbi wa Diamond Jubilee .
Mshiriki wa kinyang’anyiro hicho Waziri Salum, akifanya makamuzi jukwaani jana wakati wa kurekodi kipindi hicho kitakachorushwa hewani siku ya jumamosi saa 3: 00 usiku katika Runiga ya ITV.
Waziri Salum akiwa amembeba mshiriki mwenzake Bella Kombo mara baada ya kufuzu kuingia kwenye fainali ya shindano
Haji Ramadhani akitetea nafasi yake jukwaani hapo.
Mshiriki wa BSS Rogers Lucas akiwajibika jukwaani hapo.
Bella Kombo akionyesha uwezo wake kwa majaji wa shindano
Bella kombo, Waziri Salum na Bob Junior (kulia), wakirekodi kipindi hicho.
Msanii wa muziki wa Kizazi Kipya Salah Kaisi ‘Shaa’ akiwa katika pozi la Bella kombo katika Ufukwe wa Mbalamwezi Mikocheni jijini
Majaji wa shindano
0 comments:
Post a Comment