Social Icons

Thursday, October 20, 2011

TWANGA WAWAONJESHA WADAU UTAMU ALBAMU MPYA

Mkurugenzi wa Twanga Pepeta, Asha Baraka 'Iron Lady' akimlisha keki Jacqueline Wolper wa Bongo Movies huku Steve Nyerere akikenulia meno tukio hilo.

Juzikati wadau wa Bendi ya African Stars International 'Twanga Pepeta' walikutana ndani ya Ukumbi wa New Maisha Masaki, Dar es Salaam kwa ajili ya kusikiliza na kuangalia kideo kipya cha Wimbo wa Dunia Daraja kilichotungwa na mwimbaji mkali wa bendi hiyo, Charles Gabriel 'Chalz Baba'.
Wimbo huo ndiyo uliobeba jina la albam ya 11 ya bendi hiyo itakayozinduliwa Novemba 6, mwaka huu ndani ya Viwanja vya Leaders Kinondoni, Dar es Salaam.

Wakurugenzi wanapokutana! Asha Baraka akimlisha keki mkurugenzi wa Manywele, Maimartha Jesse huku mkurugenzi wa Bench Mark Production, Rita Paulsen 'Madam' (katikati) akishuhudia.
Bonge la keki iliyokuwa imeandaliwa kwenye shughuli hiyo.
Kiongozi wa Twanga Pepeta, Luiza Mbutu (katikati mwenye mic) akiwakaribisha wadau keki.
Kigogo wa Global Publishers, Sifael Paul 'Brother From Another Mother' (kulia) na Eric Evarist (kushoto) wakifuatilia mchakato, kwa nyuma naona...












0 comments: