Social Icons

Thursday, September 15, 2011

SOMA HISTORIA FUPI YA PAPA BENEDIKTO XVI
Papa Benedikto XVI (amezaliwa 16 Aprili 1927; jina la Kilatini: Benedictus XVI; kwa Kiitalia: Benedetto XVI) ni papa tangu 19 Aprili, 2005 baada ya kifo cha Papa Yohane Paulo II.
Ni mwandamizi wa 264 wa
Mtume Petro na Papa wa kwanza kutoka Ujerumani baada ya miaka 1000 hivi.
Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Joseph Alois Ratzinger.
Alipadirishwa tarehe 29 Juni 1951 pamoja na kaka yake Georg. Baada ya kupata udaktari katika teolojia na kufundisha miaka kadhaa, alishiriki kama mtaalamu katika Mtaguso Mkuu wa Vatikano II.
Tarehe 24 Machi
1977Papa Paulo VI kuwa Askofu mkuu wa Munchen na Frisingen akapewa daraja hiyo tarehe 28 Mei mwaka huohuo. Tarehe 27 Juni mwaka huohuo Paulo VI alimteua pia kardinali na kutokana na cheo hicho alishiriki uchaguzi wa Papa Yohane Paulo I na Yohane Paulo II mwaka 1978.
Tarehe 25 Novemba
1981 Yohane Paulo II alimteua kuwa mkuu wa Idara ya Mafundisho ya Imani. Hivyo tarehe 15 Februari 1982 aliacha uongozi wa jimbo kuu akashika kazi hiyo mpya mpaka alipochaguliwa kuwa Papa.
Katika kazi hiyo aliandaa
Katekisimu ya Kanisa Katoliki tangu 1986 hadi 1992) na Ufupisho Makini wa katekisimu hiyo tangu 2003 hadi 2005).
Baada ya kuchaguliwa Papa aliendeleza juhudi za mtangulizi wake katika utekelezaji.

0 comments: