NDEGE YAPATA AJALI MBEYA
Hii ni baadhi ya picha zinazoonyesha ndenge ilivyoharibika baada ya kupata ajali hiyo, katika eneo la Uyole pembeni kidogo ya mji wa Mbeya.
Baadhi ya abiria waliokuwemo kwenye ndenge hiyo wakisimliana na kupongezana mambo kadha wa kadha baada ya kunusulika na ajali hiyo.
Ndege hiyo ikiwa chini muda mfupi baada ya kupatwa na ajali hiyo
Mmoja wa abiria waliokuwemo kwenye ndege hiyo akichunguzwa moja ya jeraha alilopata mara baada ya kunusurika kwenye ajali hiyo.Pairoti wa ndege hiyo (kushoto), akipatiwa moja ya matibabu na askari polisi waliofika eneo la jali hiyo.
Baadhi ya wakazi wa maeneo hayo wakiwasili katika eneo la ajali tayali kwa kushuhudia tukio zima lilivyotokea.Mmoja wa abiria wa ndege hiyo akitoa maelezo namna dalili za ajli hiyo zilivyoanza hadi kutokea.
Ndege hiyo ikionekana eneo la ndani ilivyo.
AJALI ya ndege namba 9J-BIO SESINA 206, imetokea leo asubuhi majira ya saa tatu eneo la Nanenane Uyole jijini Mbeya na abiria wanne wanusurika kifo na hakuna aliyefariki.
Abiria walionusurika kifo ni pamoja JVER WAAK Umri wa Miaka 49 ambayealikuwa Rubani, Raia wa Afrika Kusini, Bwana CHRISTIAN BASIL MMASI umri miaka 30, Ambaye ni Afisa Utawala wa mashamba ya Kapunga wilaya ya Mbarali, Balozi MOHAMMED RAMIA kabula leke ni Mmakua mwenye umri wa miaka 64, mkazi wa Masaki jijini Dar es Salaam ambaye ni mfanyakazi EXPORT TRADING na Bwana SUNNY TAYIR mwenye umri wa miaka 50 ambaye ni Mhindi na ni mfanyakazi wa EXPORT TRADING.
Na chanzo cha ajali hiyo akijafahamiaka mpaka sasa.
Imetolewa na Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya Bwana Anaclet Malimbisa.
Picha/Habari kwa Hisani ya Mbeya yetu Blog
Na chanzo cha ajali hiyo akijafahamiaka mpaka sasa.
Imetolewa na Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya Bwana Anaclet Malimbisa.
Picha/Habari kwa Hisani ya Mbeya yetu Blog
0 comments:
Post a Comment