TIGO YAENDELEZA MISAADA KWENYE MASHULE SHULE DODOMA
Meneja wa Tigo kwa mikoa ya Dodoma na Singida Fadhila Saidi akimuonyesha mmoja wa wanafunzi wa Chekeckechea katika shule ya Msingi ya Kizota ya mjini Dodoma jinsi ya kutumia vibao vya kujifunzia. Jumla ya vibao 1000 vilikabidhiwa shuleni hapo na kampuni ya Tigo.
Meneja wa Tigo kwa mikoa ya Dodoma na Singida Fadhila Saidi (katikati) akimkabidhi vibao vya kujifunzia mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Kizota ya mjini Dodoma , Mwalimu Juma Malecela (kushoto). Tigo ilikabidhi vibao 1000 katika shule hiyo. Kulia ni Dotto Mwantengwe mratibu wa elimu Kata ya Kizota
Walimu wa shule ya msingi Kizota ya Dodoma Olimpia Mbuga na Felician Rocky wakiwalekeza wanafunzi jinsi ya kutumia vibao vya kujifunzia vilivyotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo. Tigo ilikabidhi jumla ya vibao 1000 katika shule hiyo
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Tigo yasaidia shule Dodoma
September 12, 2011, Dodoma, Katika jitihada zake za kusaidia sekta ya elimu nchini Tanzania , kampuni ya simu za mkononi ya Tigo imetoa msaada wa vibao vya kujifunzia 1000 kwa shule ya Msingi ya Kizota ya mjini Dodoma .
Vibao hivyo vimetengenezwa kwa kutumia plastik ili viweze kubebeka kwa urahisi. Juu ya vibao hivyo kuna michoro na maandishi ya vitu mbalimbali ambavyo vinaweza kumsaidia mwanafunzi kujifunza. Kuna michoro ya maumbo mbalimbali kama vile alfabeti, tebo ya kuzidisha na aina mbalimbali za rangi.
Kampuni ya Tigo imefikia umamuzi wa kutoa msaada huo kwa kuthamini umuhimu wa elimu ya shule ya msingi hapa nchini. Halikadhalika kwa kuzingatia kuwa watoto wa leo ndiyo watakuwa viongozi wa kesho kwahiyo ni vyema kuwaboreshea mazingira ya elimu.
Mwakilishi wa Tigo Fadhila Saidi ambaye ni meneja mauzo wa mikoa ya Dodoma na Singida alisema kuwa “Tunajisikia furaha sana kuwasaidia watoto hawa ambao ni viongozi wa kesho ili kuwarahishia njia ya kuzidi kujifunza hata kwa muda wao wa ziada na kuongezea kuwa wanafunzi anaweza kutumia vibao hivyo kujifunza vitu mbalimbali kwa wakati wake baada ya muda wa masomo.
Alisema kuwa lengo la kutoa msaada huo hasa ni kusaidia badhi ya shule za msingi hapa nchini ambazo zimekuwa zikihitaji za nyenzo za kujifunzia na kuongezea kuwa msaada huo utaendelea kutolewa katika shule nyingine za msingi hapa nchini.
“Lengo letu ni kusaidia sekta ya elimu hapa nchini na baada ya mradi huu kuna kitu kingine ambacho sisi kam Tigo tunatarajia kukifanya hivi karibuni kwa ajili ya kusaidia tena elimu hapa nchini,” alisema Fadhila.
Hivi karibuni kampuni ya Tigo iliendesha kampeni maalum ya Tigo Tuchange yenye lengo la kuchangia sekta ya elimu hapa nchini. Kiasi cha pesa kilichopatikana kitatumika kununua vitabu kwa jili ya kusaidia baadhi ya shule za msingi.
0 comments:
Post a Comment