Social Icons

Thursday, August 4, 2011

AIRTEL YATOA MSAADA WA CHEREHANI 10

Meneja Huduma za Jamii wa Airtel, Tunu Kavishe (kulia) akikabidhi moja ya mashine za kushonea, cherahani, kwa mwakilishi wa kikundi cha wanawake cha kulelea watoto yatima cha Msasani Womens and Orphans Centre, Prudencia Kibatara katika hafla ambayo Airtel ilikabidhi msaada wa vyerahani 10 kwa vikundi vitatu vya wanawake vya kulelea watoto yatima vya Msasani, Kawe na Kinondoni jijini Msasani Jijini Dar es Salaam jana.
Meneja Huduma za Jamii wa Airtel, Tunu Kavishe (kulia) akishikana mikono na motto yatima, Batuli Saidi katika hafla ambayo Airtel ilikanodhi msaada wa vyerahani 10 kwa vikundi vitatu vya wanawake vya kulelea watoto yatima vya Msasani, Kawe na Kinondoni jijini Msasani Jijini Dar es Salaam jana.
Meneja Huduma za Jamii wa Airtel, Tunu Kavishe (kushoto) akikabidhi moja ya mashine za kushonea, cherahani, kwa mwakilishi wa kikundi cha wanawake cha kulelea watoto yatima cha Msasani Womens and Orphans Centre, Yonnes Kihiyo katika hafla ambayo Airtel ilikabidhi msaada wa vyerahani 10 kwa vikundi vitatu vya wanawake vya kulelea watoto yatima vya Msasani, Kawe na Kinondoni jijini Msasani Jijini Dar es Salaam jana.

AIRTEL yatoa msaada wa cherehani 10 kwa vikundi vitatu vya watoto Yatima Dar es Saalam.
Alhamis 4 Agusti 2011, Kampuni ya simu za mikononi ya AIRTEL imetoa msaada wa vyerehani kumi kwa vikundi vitatu vya wanawake vinavyolea watoto yatima jijini Dar Es Salaam ili kuviongezea uwezo wa kulea watoto wanaolelewa katika vituo hivyo.
Msaada huo umekabidhiwa na meneja huduma za jamii wa airtel Tunu kavishe kwa vikundi hivyo. Vikubdi vilivyofaidika na msaada huo ni kikundi cha wanawake cha kulea watoto yatima cha Msasani,kikundi cha Huruma cha Kawe pamoja na kile cha kulea watoto yatima cha Kinondoni.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Bi.Kavishe alisema "AIRTEL itaendelea kugawa misaada kwa vikundi vya wasiojiweza ikiwa ni sehemu ya kampeni yake ya kusaidia jamii katika kutatua baadhi ya matatizo ambayo inayakabili hususani katika sekta ya elimu".
Akipokea msaada huo wa mashine za kushonea, mwakilishi wa kikundi cha wanawake cha kulelea watoto yatima cha Msasani Womens and Orphans Centre, Prudencia Kibatara alisema " Msaada huu utatusaidia katika kuboresha utoaji wa huduma kwa watoto hawa ambao tunawahudumia katika vituo vyetu. tunachangamoto nyingi ikiwemo idadi kubwa ya watoto na kipato kidogo cha uendeshaji vikundi hivi, hivyo tunawapongeza sana Airtel kwa kushirikiana nasi katika kusaidia jamii.
kupitia cherehani hizi tutaanzisha madarasa ya ushonaji na ada zitakazolipwa zitatumika kusaidia watoto hawa, vilevile chereharani hizi zitatumika kushona vitambaa na mashuka ambayo yataleta pato katika vikundi na tutaweza hata kuendelea kuwasomesha watoto hawa vizuri" aliendelea kusema bi Bi Kibatara Aidha Afisa mtendaji wa kata ya msasani .. Swai aliiipongeza kampuni ya simu ya Airtel kwa kujitokeza na kusaidia vikundi hivyo na kutoa angalizo kwa walezi wa vikundi hivyo kutumia msaada huo kwa manufaa ya watoto na si yao binafsi.
"Jamani wakina mama naomba huruma zetu za dhati ziendelee hakikisheni mnaendelea kutumia msaada huu mlioupata kama nyenzo ya kuendelea kuwatunza na kusaidia watoto hawa na sio kujifaidisha sisi wenyewe" alisema Afisa mtendaji wa Msasani .

..Leo Airtel wameonyesha jinsi wanavyojali jamii wanayoihudumia hivyo naomba tuwaunge mkono ili dhamira yao itimie" alimaliza kwa kusema afisa mtendaji...

Vituo vilivyopa msaada huo viko jijini Dar es salaam ambavyo kwa ujumla vyote vinalele watoto wasiopungua 40 kila kimoja. Watoto wanaolelewa katika vituo hivyo bado wanamahitaji mengi japo kampuni ya simu za mkononi airtel imeweza kujitolea msaada huo wa vyerehani bado pia wanahitaji vifaa vya shule, vifaa vya kujifunzia, chakula pamoja na malazi ya kila siku
Airtel imekuwa mstari katika kusaidia uboreshaji wa maisha ya jamii kwa kutoa misaada ya aina mbalimbali na kudhamini shughuli za miradi ya maendeleo.bado Airtel inampango wa kutoa msaada wa cherehani pia katika mikoa ya mwezi huu kwa dhumuni la kuendelea kupunguza tatizo la kipato kwa vituo vya wananchi wanaoishi katika mazingira magumu.



0 comments: