Social Icons

Thursday, August 4, 2011

PADRI AIBUKA MSHI WA MLIONI 50 ZA KWANJUKA NA AIRTEL

Afisa Uhusiano wa Kampuni hiyo Jackson Mmbando, akifafanua jambo kwa wanahabari, jinsi mchakato wa bahati nasibu hiyo ulivyokuwa ukiendeshwa na kampuni hiyo.
Mwakilishi wa idara ya Masoko Airtel Alice Paulsen (wa pili kushoto), akimwelekeza namba ya mshindi wa shindano hilo Jackson Mmbano (kulia), ili ampigie (mwanzoni kushoto), ni mmoja wa wafanyakazi wa idara hiyo, Nzelu Saharah akishuhudia zoezi hilo

Jackson Mmbando (katikati), akipiga simu ya mshindi wa bahatinasibu hiyo, tayari kwa kumpa taarifa njema (kulia), ni Mratibu wa zoezi hilo kutoka Bodi ya bahati na sibu Mrisho Milao akifahatilia zoezi hilo kwa makini na Alice Paulsen, mwanzoni kushoto.


Baadhi ya wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakishuhudia na kuchukua matukio ya zoezi hilo.




KAPUNI ya simu za mkoni Airtel Tanzania mapema leo imempata mshindi wa milioni 50 na kuongeza muda wa promiosheni hiyo kwa kipindi chote cha mwezi wa ramadhani huku ikiwa imewazawadia wateja wake jumla ya shilingi milioni 305 hadi kufikia jana,

Katika kauli iliyotolewa na meneja uhusiano wa Airtel Jackson mmbando alisema” leo tunampatia mshindi mkuu wa promotion ya kwanjuka kwa kipengele cha kwanza na pia tunaongeza muda wa promosheni pamoja na zawadi

Kuanzia sasa washindi watajishindia shilingi milioni moja kila siku na shilingi milioni 5 mwishoni mwa wiki wakati katika kilele mshindi kwenye droo kubwa ataondoka na shilini milioni 20 pesa taslim

Promosheni ya kwanjuka imeongezewa muda wa siku 31 na itahusisha wateja wote wa Airtel Tanzania watakaoshiriki =. Ili kushiriki mteja anatakiwa kutuma nene KWANJUAKA kwenda namba 15656 kisha mteja atapata maswali na akiyajibu kwa usahihi atajiongezea pointi za kuwa mshindi

Leo hii Tumefikia kilele cha promosheni hii ilipoanza tangu Aprili 2011 lakini kutokana na faida nzuri tuliyopata pamoja na wateja wetu kuipenda sana promosheni hii basi tumeamua kuongeza zawadi pamoja muda wa wateja kushiriki promosheni hii

Leo mshindi wetu wa milioni 50 droo kubwa wa sehemu ya kwanza ya promosheni hii ni Andew Isaya Goha father wa kanisa katoliki Parokia ya Mofu Mahenge Mkoani Morogoro, umri wake miaka 48

Aidha meneja wa bidhaa na mawasiliano Rahma mwapachu aliongeza kwa kusema, Airtel inawahimiza wateja kuendelea kushiriki katika shindano hili ambalo limeongezwa muda wake na linaendelea ili kupata nafasi za kujishindia zaidi mbalimbali zilizoko, tunafuraha kuwajulisha kuwa promotion hii imekuwa ya mafanikio na washindi wamepatikana kutoka sehemu mbalimbali nchini huku ikiinua maisha yao ambalo ndio lengo halisi la promosheni hii.

kampuni ya Airtel tunawaahidi watanzania kuendelea kupanua mtandao wetu zaidi ili uweze kuwafikia wanainchi wote hasa wale waishio vijijini kote nchini. Mwezi uliopita tulizidua huduma zetu kwenye zaidi ya miji na vijiji 50 ikiwa ni katika kutimiza lengo letu la kuwafikia watu wengi na kuinua kiwango cha maisha yao na nchi nzima kwa ujumla,

0 comments: