Mkazi wa Pongwe Tanga, Selina Anthony (kulia) akipima virusi vya ukimwi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji kuhusu ugonjwa wa HIV/AIDS iliyoandaliwa na kampuni ya Saruji Tanga katika mji wa Pongwe mkoani humo jana. Anayemtoa damu ni muuguzi kutoka katika…
Mkazi wa Pongwe Tanga, Selina Anthony (kulia) akipima virusi vya ukimwi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji kuhusu ugonjwa wa HIV/AIDS iliyoandaliwa na kampuni ya Saruji Tanga katika mji wa Pongwe mkoani humo jana. Anayemtoa damu ni muuguzi kutoka katika Hospitali ya Mkoa ya Bombo, Immaculata Kadaga na mtoto aliyebebwa na Selina ni mjukuu wake, Gerald Rashidi. Pichani juu: Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Saruji Tanga, David Lee (kulia) akitolewa damu kupima virusi vya ukimwi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji kuhusu ugonjwa wa HIV/AIDS iliyoandaliwa na kampuni hiyo kwa wakazi wa mji wa Pongwe mkoani humo jana. Anayemtoa damu ni muuguzi kutoka katika Hospitali ya Mkoa ya Bombo, Immaculata Kadaga.
Mkazi wa Pongwe Tanga, Hadija Rashidi (kulia) akipima virusi vya ukimwi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji kuhusu ugonjwa wa HIV/AIDS iliyoandaliwa na kampuni ya Saruji Tanga katika mji wa Pongwe mkoani humo jana. Anayemtoa damu ni muuguzi kutoka katika Hospitali ya Mkoa ya Bombo, Immaculata Kadaga.
Mkazi wa Pongwe Tanga, Zainabu Hamza (kulia) akipewa ushauri nasihi kuhusu ugonjwa wa ukimwi mara baada ya kupima damu wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji kuhusu ugonjwa wa HIV/AIDS iliyoandaliwa na kampuni ya Saruji Tanga katika mji wa Pongwe mkoani humo jana. Anayetoa ushauri ni muuguzi kutoka katika Hospitali ya Mkoa ya Bombo, Elizabeth Lawuo. Anayeangalia ni mtoto wa Selina, Amina Adamu.
Na Mwandishi Wetu, Pongwe Tanga
KAMPUNI ya Saruji Tanga imezindua kampueni ya siku nne kuhusu masuala ya ufahamu juu ya ugonjwa wa HIV/AIDS na upimaji wa virusi vya ugonjwa huo katika kata ya Pongwe mkoani Tanga jana ikiwa ni sehemu ya sera za kampuni hiyo katika kuisaidia jamii (CSI).
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tanga Cement, David Lee alisema Tanga Cement imeona kuna umuhimu mkubwa wa kufanya kampeni hiyo kwani maendeleo ya Taifa lolote yanatokana na kuwa na watu wenye afya bora.
“Tanga Cement inajenga Tanzania, hivyo tunaamini kuwa huwezi kujenga Taifa kama wananchi wengi watakuwa hawana afya hususani vijana ambao ndio nguvu kazi kubwa katika uchumi wan chi hii”, akasema.
Mkurugenzi huyo alisema kampeni kama hiyo ilianzia kwanza kwa wafanyakazi wao pamoja na familia zao katika mkakati huo huo kwamba ugonjwa wa ukimwi unazorotesha afya hivyo kampuni haitaweza kutimiza malengo yake endapo idadi kubwa ya wafanyakazi watakuwa ni waathirika.
“kama ilivyo kauli mbiu yetu katika kampeni hii kuwa ’Okoa Maisha Pima Afya yako’ hivyo tunaamini ukijua hali yako ukiwa umeathirika au hujaathirika itakusaidia kujiokoa wewe, familia yako na wale wanaokuzunguuka”, akaongeza.
Akizungumzia utekelezaji wa zoezi hilo, Ofisa Mawasiliano wa TCCL, Bi. Mtanga Noor alisema wanatarajia kuhudumia zaidi ya wakazi 600 katika eneo hilo la Pongwe na kijiji cha Kichangani vyote vikilizunguuka eneo ya kiwanda na makazi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo.
“Hawa majirani zetu hivyo afya zao ni muhimu pia na ndio sababu moja ya vipengele tunavyoangalia katika mpango wetu wa kuisaidia jamii (CSI) ni afya, na ukimwi unaingia katika kipengele hiki”, akasema.
Bi. Mtanga akasema katika kampeni hiyo ya siku nne wananchi hao watapata ushauri nasihi kuhusu ugonjwa huo, kuchunguzwa afya zao ambapo zaidi ya shs milioni 17 zitatumika kufanikisha zoezi hilo.
Awali akizungumzia hali ya ugonjwa huo Mratibu Ukimwa mkoani humo, Moses Kisibo aliishukuru Tanga Cement kwa kufanikisha zoezi hilo litakalosaidia kupunguza kasi ya maambukizi katika Mkoa wa Tanga akisema kuwa kwa sasa ipo zaidi ya aslimia 8.7
Mratibu huyo alitaja moja ya sababu inayochangia kuongezeka kwa kasi ua ugonjwa huo kuwa ni uelewa mdogo kuhusu HIV/AIDS kwa wakazi wa mkoa huo ambapo zaidi ya asilimia 75 ya watu wanaojijihusisha na masuala ya ngono wanafanya ngono za gizani.
“Kondomu hazitumiki watu wanafanya ngono ‘gizani’ na hata hao wanaozitumia hawazitumiii jinsi inavyotakiwa kwa kufuata hatua zinazoshauriwa na wataalamu hii inachangia kasi ya ugonjwa huu kuwa kubwa”, akaongeza.
Mmoja wa wakazi waliojitokeza kupima virusi vya ukimwi yeye na mtoto wake, Zainabu Hamza na mwanaye, Amina Adamu alisema anafuraha sana baada ya kujitambua afya yake kwani hiyo ilikuwa mara yake ya tatu hivyo hiyo itamsaidia kuweza kuishi akichukuja tahadhari zote ili asipate maambukizi.
0 comments:
Post a Comment