Baadhi ya washiriki wa kinyang’anyiro hicho wakiwa kwenye pozi leo mchana.
Benny Kisaka akihesabu sehemu ya pesa zinazotarajiwa kutolewa zawadi kwa washiriki hao.
MKURUGENZI wa BMP Promotions inayoratibu Shindano…
Baadhi ya washiriki wa kinyang’anyiro hicho wakiwa kwenye pozi leo mchana.
Benny Kisaka akihesabu sehemu ya pesa zinazotarajiwa kutolewa zawadi kwa washiriki hao.
MKURUGENZI wa BMP Promotions inayoratibu Shindano la Miss Temeke, Benny Kisaka, leo amesema mrembo atakayeibuka na Taji la Miss Temeke katika mpambano unaotarajiwa kufanyika Jumamosi ijayo ndani ya Ukumbi wa TCC Chang’ombe jijini Dar es Salaam, atazawadiwa kitita cha shilingi milioni mbili.
Kisaka ametoa ahadi hiyo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Hoteli ya Court Yard jijini Dar es Salaam.
Mwandishi wa habari wa Redio Uhuru, Cesi Jeremiah (kushoto) akitaka kufafanuliwa jambo katika mkutano huo. Kulia ni mwandishi wa Jambo leo, Asha Kigundula.
Warembo walioapa kunyakua taji hilo, kutoka kushoto ni: Naifat Ally, Prisca Steven, Sarah Said, Irene Jackson na Eunice Mbuya.
Kisaka akizungumza na washiriki baada ya mkutano na wanahabari.
Miss Temeke mwaka 2000, Irene Kiwia, akiwatia moyo washiriki hao.
Prisca Steven, akionesha uso wa tabasabu wakati akifotolewa na paparazi wetu.
0 comments:
Post a Comment