Social Icons

Wednesday, July 13, 2011

MBUNGE WA IGUNGA VIJIJINI, ROSTAM AZIZ AJIUZURU RASMI

MBUNGE wa Jimbo la Igunga, Rostam Azizi leo ametangaza rasmi mbele ya wapiga kura wake kujivua nyadhifa zake zote alizozipata kupitia Chama cha Mapinduzi.
Akihutubia huku akikatishwa na kelele za wapiga kura wake zilizokuwa zikipingana na uamuzi huo Rostamu amesema uamuzi wake huo hautokani na shinikizo la mtu, kundi la watu au Chama bali ni dhamira yake mwenyewe ya kutaka kuachana na siasa uchwara na kuamua kusimamia vyema biashara zake.
"Naomba niliweke hili wazi....narudia tena naomba niliweke hili wazi kuwa uamuzi wangu huu hautokani na shinikizo lolote kutoka kwa mtu yeyote bali ni dhamira yangu ya dhati ya kutaka kuachana na siasa hizi uchwara ili nisimamie biashara zangu kikamilifu" alisema Rostam.

0 comments: