MTANZANIA Steven Konyaki (pichani) mkazi wa Sinza ya Palestina, jijini Dar es Salaam ambaye kwa sasa anaishi Marekani, amefikishwa kortini nchini humo akidaiwa kumbaka bibi kizee mwenye umri wa miaka 62.
Kwa mujibu wa mashtaka kupitia mtandao mmoja nchini humo, Steven alitenda kosa hilo nyumbani kwake Mtaa wa Hamley jijini Lynn, Massachusetts na kuripotiwa polisi Novemba 4, 2010.
Kwa mujibu wa maelezo ya polisi ya bibi kizee huyo, siku ya tukio alikwenda kumtembelea rafiki yake wa kike ambaye anaishi nyumba moja na Konyaki.
Maelezo hayo yalidai kuwa, akiwa hapo mtuhumiwa huyo alimbaka kitandani chumbani kwake hali iliyomfedhehesha.
Katika maelezo yake ya utetetezi aliyoyatoa kituo cha polisi, Steven alisema kuwa, siku hiyo alikuwa amelewa sana hivyo hakujua alilokuwa akilifanya.
Akiendelea kudai kwamba, wakati anafanya mapenzi na bibi kizee huyo alijua ni msichana mwenye miaka 16.
Mtuhumiwa alipandishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Lynn na kusomewa mashitaka hayo.
Aliachiwa huru kwa dhamana ya Dola za Kimarekani 1,500 (karibu shilingi milioni tatu za Kibongo) huku kesi yake ikiendelea kufanyiwa upelelezi wa kina.
Mei 25 mwaka huu, Steve alipandishwa tena Mahakama Kuu ya Salem mbele ya jopo la majaji likiongozwa na Jaji, Howard ambapo alisomewa tena mashtaka yake.
Kwa mujibu wa sheria za Marekani, endapo Konyaki atakutwa na hatia anaweza kuhukumiwa kifungo cha miaka 20 jela.
Kesi hiyo, ilitarajiwa kusikilizwa tena jana, (Juni 15) katika mahakama hiyo.
Nchini Tanzania, jijini Dar es Salaam mwandishi wetu alikwenda nyumbani kwa wazazi wa Steven maeneo ya Sinza, Palestina na kukutana na wazazi wa mtuhumiwa huyo ambao walikiri kuwa na taarifa hizo.
Hata hivyo, mdogo wa mshitakiwa aitwaye Paul Konyaki alipingana na tuhuma hizo akidai kuwa, kuna wabaya wamembambikiza kesi Steven.
“Yaani hizo taarifa ni za siku nyingi sana, hivi ninavyokwambia hata kesi yenyewe imeisha kwa sababu yule aliyekwenda kushtaki alijua makosa yake kuwa, alimbambikia kosa ambalo si la kwake.
“Tukio lilikuwa hivi, Steve alikuwa na marafiki zake wakiwa wanakunywa pombe na kila mmoja alikuwa na mpenzi wake.
“Mara rafiki yake mmoja akamshutumu Steve kuwa anatoka na mwanamke wake, Steve akapata hasira na kumwambia ni kweli ndipo yule rafiki yake akaenda kuwachukua polisi na kumbambikia kuwa alibaka,” alisema Paul.
0 comments:
Post a Comment