Mwandishi wetu alikuta kundi la mbuzi wakiranda ndani ya uwanja huo bila kubughudhiwa na mtu yeyote huku wakizitafuna nyasi za uwanja huo watakavyo.
Hata hivyo, mbuzi hao walionekana kuwa kero kwa timu za soka na netiboli za jeshi la polisi Mkoa wa Morogoro zilizokuwa zikifanya mazoezi katika uwanja huo ambapo mara kwa mara mbuzi hao waliingia kwenye maeneo ya michezo hiyo na kusababisha usumbufu kwa wanamichezo hao.
Uchunguzi wa haraka uliofanywa na matandao huu umeshindwa kubaini mmiliki wa mbuzi hao na nani aliyewaingiza ndani ya uwanja huo.
Juhudi za mwandishi wetu za kutaka kuzungumza na meneja wa uwanja huo, Herman Ndissa, kuhusiana na mbuzi hao ziligonga mwamba baada ya kukuta kufuli likining'inia kwenye mlango wa ofisi zake katika uwanja huo unaomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Morogoro.
0 comments:
Post a Comment