Ofisa Uhusiano wa Tigo Tanzania, Jackson Mmbando (wa kwanza kulia) akitaja majina ya washindi wa bahati nasibu hiyo. Wengine pichani ni Meneja Matangazo wa Tigo, Imelda Jerald (katikati) na Afisa Huduma za Ziada wa Tigo, Pamela Shelukindo (wa kwaza kushoto).
KAMPUNI ya simu za mikononi ya Tigo leo imekabidhi mifano ya hundi kwa washindi mbalimbali waliopatikana kutokana na bahati nasibu ya Bahatika na Tigo inayoendeshwa na kampuni hiyo. Makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi za makao makuu ya kampuni hiyo zilizopo mtaa wa Lugoda jijini Dar es Salaaam.
Meneja Matangazo wa Tigo, Imelda Jerald (kulia) akimkabidhi Rose Ngowi mfano wa hundi ya shilingi laki saba na nusu.
Meneja Matangazo wa Tigo, Imelda Jerald akimkabidhi Robert Leata mfano wa hundi ya shilingi laki tano alizojishindia.
Salim Abdallah, mshindi wa shilingi milioni moja akionesha mfano wa hundi aliyokabidhiwa.
Meneja Matangazo wa Tigo, Imelda Jerald (kulia) akimkabidhi Idd Kibwana mfano wa hundi ya shilingi milioni moja.
Mariam Hamis (kulia) na Said Kisuda ambao ni washindi wa hundi ya shilingi milioni mbili kila mmoja wakiwa katika picha ya pamoja na mfano wa hundi hiyo.
PICHA NA IMELDA MTEMA/GPL
0 comments:
Post a Comment