Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanoa Dk. Mohamed Gharib Bilal (katikati), kulia Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Abbott Fund Tanzania Andy Wilson, kushoto Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. John Mwakipesile, wakikata utepe kuzindua kituo cha huduma za tiba kwa ajili ya watoto walioathirika na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi Mkoani Mbeya leo, kituo hicho kimejengwa kwa msaada wa mfuko wa Abbott Fund kutoka Marekani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal, akiangalia baadhi ya vifaa vya kupimia virusi vya Ukimwi baada ya kufungua kituo cha kutolea tiba kwa walioathirika na Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi Mkoani Mbeya leo kilichojengwa kwa msaada wa Shirika la Kimataifa la Abbott Fund la Marekani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal akizungumza na Msaidizi Mkuu wa Balozi wa Marekani Nchini Robert Scot na Makamu wa Rais wa Shirika la kimataifa la Abbott Fund la Marekani Andy Wilson baada ya kufungua kituo cha huduma za tiba kwa walioathirika na maambukizi ya virusi vya Ukimwi mkoani Mbeya leo. kushoto Waziri wa Afya Mhe. Haji Mponda.
Dk. Mohamed Gharib Bilal katikati, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa shirika la kimataifa la Abbott Fund la Marekani na viongozi wa Mkoa wa Mbeya baada ya kufungua jengo la kituo cha huduma za tiba kwa walioathirika na maambukizi ya virusi vya Ukimwi mkaoni Mbeya leo.
Picha zote na Amour Nassor / Ofisi ya Makamu wa Rais
0 comments:
Post a Comment